Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Watenegenezaji, waingizaji dawa feki za asili kusakwa, NIMR kufungua kiwanda

Дата публикации: 28-08-2026 16:18:59

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limetangaza kuanza msako wa kubaini dawa zinazoingizwa nchini kinyemela bila kufuata sheria, huku likiwatafuta watengenezaji wa bidhaa hizo kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

Основное содержимое страницы с новостью.

Ijumaa, Agosti 28, 2026

Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, (NIMR), Profesa Said Aboud akizungumza jijini Mbeya wakati wa kongamano la tano la kisayansi la tiba asili. 

By  Sadam Sadick

Mwananchi Communications Limited

Muktasari:
  • Hatua hiyo imekuja baada ya baraza hilo kubaini kuwepo kwa dawa aina ya kusisimua mwili iliyoingizwa nchini kutoka Malaysia bila kupata uthibitisho kutoka mamlaka husika, ikiwamo Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).

Mbeya. Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limetangaza kuanza msako wa kubaini dawa zinazoingizwa nchini kinyemela bila kufuata sheria, huku likiwatafuta watengenezaji wa bidhaa hizo kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

Hatua hiyo imekuja baada ya baraza hilo kubaini kuwepo kwa dawa aina ya kusisimua mwili iliyoingizwa nchini kutoka Malaysia bila kupata uthibitisho kutoka mamlaka husika, ikiwamo Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).

Akizungumza leo Ijumaa, Agosti 28, 2026, wakati wa Kongamano la Tano la Kisayansi la Tiba Asili, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Profesa Joseph Otieno amesema kuna dawa zinazoingia nchini bila kufuata taratibu za kisheria na kwamba, Serikali inaendelea na msako kubaini uingizwaji wa bidhaa hizo.

Amesema Baraza lina jukumu la kusajili na kusimamia dawa zote za tiba asili na tiba mbadala zinazotumika kwa binadamu, kwa kushirikiana na taasisi nyingine ikiwemo NIMR katika utafiti na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

“Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala ya mwaka 2002 hairuhusu kutoa dawa ya asili ambayo haijasajiliwa. Kama mtu hataki kujisajili au kusajili bidhaa zake, asiingie kwenye tasnia kwa kuwa ni kinyume cha sheria,” amesema.

Amesema mwezi uliopita walibaini dawa iliyotoka Malaysia ikiwa kwenye soko la Tanzania na kuipiga marufuku, huku wakimtafuta mtengenezaji wake.

“Kuna dawa nyingine zinaingia bila kupita kwetu. Mwezi uliopita kuna dawa ilitoka Malaysia. Tulipoikuta sokoni tumeipiga marufuku na tunamtafuta mtengenezaji. Tumebaini zipo dawa zinaingia kimagendo na tunafuatilia,” amesema Profesa Otieno.

Amesema ili kudhibiti hali hiyo, baraza limeanza mkakati wa kutambua dawa, maduka na watengenezaji wake ili kuhakikisha bidhaa hizo zinasimamiwa ipasavyo.

“Hadi sasa tumesajili dawa 200 na kati ya hizo tumepeleka 20 kwenye huduma jumuishi. Tunafuatilia soko na mtengenezaji kujua matumizi yake yakoje kulingana na usajili, vinginevyo tunachukua hatua,” amesema.

NIMR kufungua kiwanda

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Profesa Said Aboud amesema kutokana na mahitaji ya dawa za asili zenye ubora na ufanisi, taasisi hiyo inatarajia kufungua rasmi kiwanda chake kilichopo Mabibo, Dar es Salaam, mwaka huu.

Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya tiba ya mifupa na ubongo Balozi, Dk Mpoki Ulisubisye

Amesema Serikali imewekeza katika ujenzi wa kiwanda hicho na kwamba katika mwaka wa fedha 2026/27, NIMR inatarajia kukamilisha hatua za mwisho na kuanza kukitumia.

“Kiwanda hiki si kwa ajili ya NIMR tu, bali pia kwa wazalishaji wengine wasio na maeneo ya uzalishaji. Nawaomba wote kujiandaa kutumia fursa hii na kuimarisha ubora wa dawa zao,” amesema.

Profesa Aboud amesema utafiti katika tiba asili bado ni mdogo ukilinganishwa na tafiti nyingine za afya, akitaja uhaba wa rasilimali fedha kuwa miongoni mwa sababu.

Amesema NIMR inaendelea kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto hiyo ili kuongeza tafiti zitakazosaidia kuboresha tiba asili nchini.

Akifungua kongamano hilo kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Emmanuel Tayari, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo (MOI), Balozi Dk Mpoki Ulisubisya amesema Wizara imeimarisha ufuatiliaji wa dawa za asili.

“Tunasimamia mifumo bora ya utekelezaji na kuongeza uwezo wa maabara kupima ubora wa bidhaa za tiba za asili. Lazima tuongeze jitihada za kuwafundisha wataalamu wa tiba asili ili jamii ipate huduma inayofaa kiutamaduni na iliyothibitishwa kisayansi,” amesema.

Amesema Serikali haitaruhusu tiba za asili zinazoweza kuleta madhara kwa watumiaji, akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha tiba hizo zinazingatia usalama, ubora na viwango vinavyotakiwa.

“Tiba asili ni sehemu ya urithi wetu kiutamaduni na fahari kitaifa, ujuzi ambao umelelewa na jamii kwa karne nyingi,” amesema.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1KCMC yaitaka NIMR kuharakisha ‘One-Stop Centre’08.9628-08-2026
2Минздрав готовит новое распоряжение о ввозе незарегистрированных лекарств0023-01-2020
3Tanzania warns fake input dealers, fertiliser smugglers of tough action0511-07-2026
4Росалкогольрегулирование получило доступ к данным о производстве спиртосодержащих лекарств0020-07-2022
5Мурашко: нужно принимать меры в отношении производителей, резко снижающих выпуск лекарств0008-12-2020
6CAG Kichere azishukia halmashauri tano Mara, atishia...06.0928-08-2026
7Дума отменила декриминализацию ввоза незарегистрированных в РФ лекарств из перечня ВОЗ0022-03-2023
8Россельхознадзор выступил за запрет работы предпринимателей, замеченных в контрафакте0016-06-2021
9Аптеки пожаловались в Роскомнадзор на Ozon.ru за онлайн-торговлю лекарствами0024-10-2018
10Разрешение на дистанционную продажу лекарств в РФ получили более 300 аптечных организаций0012-03-2021

Классификация: Экономика. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 7.71. Источник: www.mwananchi.co.tz.