Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Wachezaji Harambee Stars wagomea mazoezi kisa posho

Дата публикации: 24-09-2026 14:28:19

Wachezaji wa timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’, wamegoma kufanya mazoezi wakilalamikia kutolipwa posho zao za kambi zilizopita.

Основное содержимое страницы с новостью.

Nairobi. Wachezaji wa timu ya taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’, wamegoma kufanya mazoezi wakilalamikia kutolipwa posho zao za kambi zilizopita.

Hatua hiyo imeibua mvutano ndani ya timu hiyo, ikiwa zimesalia siku chache kabla ya Kenya kukutana na Eritrea katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi.

Kocha Mkuu wa Harambee Stars, Benni McCarthy, amethibitisha kuwepo kwa mgogoro huo, akieleza kuwa hali ya sasa imeathiri morali ya wachezaji na maandalizi ya timu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wachezaji wamekuwa wakidai malipo ya posho ambazo hawakupokea katika kambi zilizopita, huku pia wakilalamikia pia mazingira ya kambi kuwa yasiyoridhisha wakati wa maandalizi.

Mgomo huo umezidisha shinikizo zaidi kwa benchi la ufundi na viongozi wa soka nchini Kenya, ambao sasa wanakabiliwa na jukumu la kutatua suala hilo kabla ya mchezo dhidi ya Eritrea.

Mechi hiyo ni sehemu ya safari ya Harambee Stars kuelekea AFCON 2027, hivyo maandalizi ya timu yanatarajiwa kuwa muhimu katika kuhakikisha wachezaji wanaingia uwanjani wakiwa tayari kiushindani.

McCarthy ameeleza kuwa, kushuka kwa morali ya wachezaji wakati huu kunaweza kuathiri maandalizi ya timu, huku jitihada zikiendelea kurejesha utulivu ndani ya kikosi.

Mkuu wa Miradi na Timu za Taifa wa Shirikisho la Soka Kenya(FKF), Athanus Obango amekiri wachezaji kudai malimbikizo ya posho, ambazo ni KSh 80,000(Sh2 milioni), kila mmoja za mechi dhidi ya Senegal na Lesotho, lakini akaitupia Serikali ya Kenya kuwa ndio yenye jukumu la kuwalipa.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Ngorongoro yapoteza kwa penalti fainali CECAFA-2008.6424-09-2026
2Taifa Stars yapoteza nyumbani, hesabu zahamia kwa Madagascar.01025-09-2026
3Нестеров: сборной России нужно реабилитироваться за поражение от чехов на Кубке Карьяла0012-12-2018
4Галактионов: российские футболисты на молодежном Евро должны отталкиваться от своей игры0015-03-2021
5ФК "Спартак" возобновит тренировки в понедельник0015-11-2020
6Shalulile apewa onyo kali Yanga01024-09-2026
7Сборная России в полном составе проводит тренировку перед играми отбора на чемпионат мира0005-10-2021
8Риск недооценки есть. Сборная России по футболу готовится к матчу против команды Кипра0009-11-2021
9Футболисты "Спартака" Кофрие, Маслов и Понсе тренируются по индивидуальной программе0024-01-2022
10Việt Nam step up preparations for Asian Games012.3519-08-2026

Классификация: Спорт. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 5.92. Источник: www.mwananchi.co.tz.