Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Mwanafunzi wa darasa la saba auawa Songwe

Дата публикации: 20-07-2026 16:45:06

Kamanda Senga amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu matukio hayo, sambamba na msako wa kuwabaini na kuwakamata wahusika ili wafikishwe mahakamani.

Основное содержимое страницы с новостью.

Songwe. Mwanafunzi wa darasa la saba, Simoni Mwamlima (15), ameuawa katika tukio lililotokea Kitongoji cha Chang'ombe, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe, huku Jeshi la Polisi likiendelea na msako wa kuwabaini na kuwakamata watu wanaohusishwa na mauaji hayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, Julai 20, 2026, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga, Simoni, aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Ntungwa, alikutwa akiwa na jeraha la kukatwa kwa kitu chenye ncha kali nyuma ya shingo.

Kamanda Senga amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa Simoni aliondoka nyumbani kwao Julai 17, 2026, saa 2:00 usiku, akielekea dukani kununua betri za tochi, lakini hakurejea hadi mwili wake ulipopatikana siku iliyofuata.

Amesema tukio hilo ni miongoni mwa matukio mawili ya mauaji yaliyotokea katika wilaya za Momba na Mbozi, ambayo Jeshi la Polisi linaendelea kuyafanyia uchunguzi.

“Katika tukio la pili, lililotokea Julai 19, 2026, saa 7:30 mchana, katika Kitongoji cha Nzije A, Kata ya Halungu, Wilaya ya Mbozi, George Songa (55) aliuawa akiwa ndani ya nyumba yake baada ya kushambuliwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na kwenye mkono wa kulia,” amesema.

Kamanda Senga amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu matukio hayo, sambamba na msako wa kuwabaini na kuwakamata wahusika ili wafikishwe mahakamani.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linaendelea na uchunguzi wa matukio haya huku likiwasaka watuhumiwa. Tunatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana nasi kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kuwabaini na kuwakamata wahusika ili wachukuliwe hatua za kisheria,” amesema Kamanda Senga.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Wahadhiri vyuo vikuu watoa tamko kupinga kamatakamata0520-07-2026
2СК проверяет обстоятельства гибели студента из Камеруна в Калининграде0515-07-2026
3Chanzo ghorofa kupigwa mnada kwa mkopo wa Sh10 milioni0520-07-2026
4Полиция Москвы проводит проверку по заявлению о пропаже кубинского студента0027-01-2021
5Kutoka 'ombaomba' hadi kumiliki bajaji2620-07-2026
6Осужденный за нападение на полицейских студент из США не будет просить о помиловании0028-06-2021
7В полиции Кении заявили, что убийство депутата Вере было "преднамеренным"0001-05-2025
8МВД Белоруссии пообещало разобраться со случаями насилия со стороны милиции0016-08-2020
9Следовали допрашивают подозреваемого в убийстве полицейского в Москве0003-09-2018
10Polisen hittar inte någon anmälan om misstänkt mutbrott0518-06-2026

Классификация: Международные. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 5. Источник: www.mwananchi.co.tz.