Rais Samia amesisitiza kuwa kupanua biashara na uwekezaji ni muhimu katika kutumia fursa zilizopo na kuhakikisha wananchi wa Tanzania na Misri wananufaika zaidi na uhusiano wa nchi hizo.
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa Tanzania na Misri kuongeza biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo ili kutumia kikamilifu fursa zilizopo na kuongeza manufaa kwa wananchi wa pande zote mbili.
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Ijumaa, Agosti 28, 2026, alipokutana na Balozi wa Misri nchini Tanzania, Sherif Ismail aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam kumuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa miaka minne wa uwakilishi nchini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, mazungumzo ya viongozi hao yalijikita katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Misri katika maeneo mbalimbali.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Sherif Ismail, Balozi wa Misri anayemaliza muda wake nchini Tanzania leo Agosti 28, 2026, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa nchi hizo zimeendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji, elimu, afya, kilimo, nishati, utalii, usafiri na uchukuzi, pamoja na maeneo mengine.
Rais Samia amesisitiza kuwa kupanua biashara na uwekezaji ni muhimu katika kutumia fursa zilizopo na kuhakikisha wananchi wa Tanzania na Misri wananufaika zaidi na uhusiano wa nchi hizo.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Sherif Ismail, Balozi wa Misri anayemaliza muda wake nchini Tanzania leo Agosti 28, 2026, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katika sekta ya usafiri na uchukuzi, viongozi hao wamejadili umuhimu wa kuboresha miundombinu na huduma ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na kuongeza biashara kati ya Tanzania na Misri, pamoja na kufungua fursa zaidi katika masoko mengine ya Afrika.
Mbali na masuala ya biashara na uwekezaji, Rais Samia ameishukuru Serikali ya Misri kwa kuendelea kutoa fursa za masomo, mafunzo na programu mbalimbali za kuwajengea uwezo Watanzania.

Afya ni miongoni mwa maeneo yaliyojadiliwa, huku pande hizo zikieleza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika mafunzo kwa wataalamu wa afya, upatikanaji wa vifaa tiba pamoja na uzalishaji wa dawa.
Kwa upande wake, Balozi Ismail amemshukuru Rais Samia, Serikali na wananchi wa Tanzania kwa ushirikiano, msaada na ukarimu alioupata katika kipindi chote cha miaka minne aliyohudumu nchini.
“Muda wangu wa utumishi Tanzania umekuwa sehemu muhimu na ya kukumbukwa katika maisha yangu ya kidiplomasia. Urafiki kati ya Tanzania na Misri utaendelea kudumu,” amesema.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Мишустин предложил активнее сотрудничать в ЕАЭС по креативным проектам | 0 | 13.61 | 05-08-2026 |
| 2 | Президент Эритреи предложил создать план сотрудничества РФ и Африки к следующему саммиту | 0 | 0 | 28-07-2023 |
| 3 | Tanzania, DR Congo Deepen Trade, Mining Ties | 0 | 6.55 | 19-08-2026 |
| 4 | Tanzania-Saudi Put 1.32tri/ - Projects On Table | 0 | 11.49 | 18-08-2026 |
| 5 | Ndejembi athibitishwa kwa asilimia 100, aahidi utii kwa Rais Samia | 0 | 8.88 | 28-08-2026 |
| 6 | Мишустин: укрепление интеграции в Союзном государстве будет ответом на санкции Запада | 0 | 0 | 02-02-2023 |
| 7 | РФ и Таджикистан договорились об активизации контактов между деловыми кругами | 0 | 0 | 09-10-2025 |
| 8 | Мишустин предложил дать поручение о подготовке новых совместных проектов РФ и Казахстана | 0 | 0 | 18-08-2021 |
| 9 | Мирзиёев инициировал "Агроэкспресс Центральная Азия - РФ" для роста товарооборота | 0 | 0 | 09-10-2025 |
| 10 | Лавров и глава МИД Замбии обсудили развитие торгово-экономических связей | 0 | 0 | 24-11-2022 |