Bunge limemthibitisha Makamu wa Rais mteule, Deogratius Ndejembi kwa asilimia 100, huku mwenyewe akisema dhamana aliyopewa haitapimwa kwa ujana wake, bali utii kwa mkuu wa nchi na uadilifu kwa Watanzania.
Dar es Salaam. Bunge limemthibitisha Makamu wa Rais mteule, Deogratius Ndejembi kwa asilimia 100, huku mwenyewe akisema dhamana aliyopewa haitapimwa kwa ujana wake, bali utii kwa mkuu wa nchi na uadilifu kwa Watanzania.
Ndejembi amethibitishwa na Bunge, baada ya Rais Samia Suluhu Hassan, kupendekeza jina lake kuwa Makamu wa Rais, kumrithi Dk Emmanuel Nchimbi, aliyeandika barua ya kujiuzulu Agosti 25, 2026.
Sambamba na barua hiyo, Agosti 26, mwaka huu Chama cha Mapinduzi (CCM), kilimfukuza uanachama Dk Nchimbi baada ya tuhuma za maadili na ukiukwaji wa Katiba ya chama hicho.
Mchakato wa kuthibitishwa kwa Makamu wa Rais mteule, umefanyika bungeni jijini Dodoma leo, Agosti 28, 2026. Kura zilizopigwa ni 324 na zote zilikuwa za ndio, hakukuwa na hapana wala iliyoharibika.

Katika hotuba yake ya shukurani baada ya kuthibitishwa Ndejembi, amesema ukubwa wa dhamana hiyo hautapimwa kwa ujana wake, bali kwa utii kwa Rais, uadilifu kwa Watanzania, kazi yoyote atakayotumwa kuitekeleza na mkuu wa nchi.
Ameeleza imani iliyoonyesha na wajumbe wa Halmashauri Kuu ni ishara kwamba CCM inawalea na inawapika vijana ili kushika uongozi ndani ya nchi.
Ndejembi amesema amezaliwa na kukua ndani ya CCM, akishika nafasi mbalimbali ndani yake na hata serikalini, hivyo anashukuru.
Ameeleza anakwenda kuwa Makamu wa Rais siyo wa Wana CCM pekee, bali vyama vyote na Watanzania kwa ujumla kama ilivyo kwa Rais wa nchi.
“Nitajitahidi kwa unyeyekevu mkubwa sana, kumsaidia Rais kuwa kiungo kwa Watanzania wote. Kama vile mapenzi yake yatakavyotaka kwa sababu nafanya kazi chini ya Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Ndejembi.
Makamu huyo wa rais mteule, amesema uteuzi aliopewa ameonyeshwa wema na ataulipa kwa utu kwa kuwa mtiifu kwake na atalipa imani aliyopewa na bunge kutekeleza majukumu yake kutimiza malengo ya Watanzania.
Amemshukuru Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba kwa malezi yake kwa kuwa alikuwa akifanya kazi chini yake na anatarajia kuendelea kupata ushirikiano wake katika utekelezaji wa majukumu yake.

“Pia, nina imani ushirikiano utakuwa mkubwa Mwananchi mwenzangu (Mshabiki wa Klabu ya Soka ya Yanga) vilevile,” amesema na kuibua vicheko kutoka kwa wabunge.
Amewaahidi wananchi wenzake wa Chamwino alikokuwa akiwatumikia kwa nafasi ya ubunge, akisisitiza kwa jambo lolote wasisite kumshirikisha watalitatua kwa pamoja.
Ametaka mshikamano ili kuhakikisha Watanzania wayapate yale wanayoyahitaji kwani Serikali imetoa fedha nyingi za kutekeleza miradi mbalimbali.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Mfahamu Dk Nchimbi aliyejiuzulu makamu wa rais | 0 | 10 | 26-08-2026 |
| 2 | ЦИК Замбии заявил о переизбрании действующего президента на второй срок | 0 | 8.16 | 18-08-2026 |
| 3 | В Танзании оппозиция не признала результатов президентских выборов | 0 | 0 | 31-10-2020 |
| 4 | Rais Samia ataka Tanzania, Misri kuongeza biashara | 0 | 5.52 | 28-08-2026 |
| 5 | Samia Suluhu Hassan Hails Hichilema's Zambia Re-Election Victory | 0 | 13.67 | 19-08-2026 |
| 6 | Zambia Election - Tanzania Denies Meddling | 0 | 9.47 | 17-08-2026 |
| 7 | Президента Замбии Хичилему переизбрали на второй срок | 0 | 9.2 | 18-08-2026 |
| 8 | Kilio cha abiria Stendi ya Magufuli chaanza kutatuliwa | 0 | 10 | 28-08-2026 |
| 9 | Президента Замбии переизбрали на второй срок | 0 | 14.93 | 18-08-2026 |