Wakati magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na saratani yakizidi kuwa changamoto katika jamii, kuna haja ya kuanza kufikiria upya mahali elimu ya kinga dhidi ya magonjwa hayo inapopaswa kuanzia.
Mwanza. Wakati magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na saratani yakizidi kuwa changamoto katika jamii, kuna haja ya kuanza kufikiria upya mahali elimu ya kinga dhidi ya magonjwa hayo inapopaswa kuanzia.
Licha ya magonjwa haya kuleta madhara makubwa kiafya duniani, bado elimu ya kujikinga nayo inaonekana zaidi kama jambo la watu wazima.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari, shinikizo la juu la damu na mengineyo, husababisha takribani vifo milioni 41 kila mwaka duniani, sawa na asilimia 74 ya vifo vyote. Kati ya hivyo, milioni 17 hutokea kwa watu walio chini ya miaka 70.
Tatizo hili lina uzito zaidi katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati, ambako zaidi ya robo tatu ya vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyoambukiza hutokea. Pia shirika linasema asilimia 86 ya vifo vya mapema vinavyotokana na magonjwa hayo hutokea katika nchi hizo.
Tuchukue hatua
Kwa Tanzania takwimu hizo zinapaswa kutufanya tujiulize je, tunaanza kuwafundisha watoto kujikinga na magonjwa haya wakati unaofaa?
WHO inaeleza kuwa vihatarishi vikuu vya magonjwa yasiyoambukiza ni matumizi ya tumbaku, kutofanya mazoezi, lishe isiyofaa, matumizi hatarishi ya pombe na uchafuzi wa hewa.
Muhimu zaidi, shirika hilo linaeleza kuwa tabia nyingi zinazohusiana na lishe, mazoezi na matumizi ya vilevi, hujengwa wakati wa utoto na ujana.
Kitakwimu zaidi ya watoto bilioni 2.3 walio katika umri wa kwenda shule, hutumia takribani theluthi moja ya muda wao shuleni.
Hivyo, shule ni mazingira muhimu ya kuwafikia watoto wengi na kuwajengea mitindo ya maisha yenye afya.
WHO pia inasema shule zinapaswa kuwa sehemu ya kukuza afya, kupitia sera za shule, mazingira salama na yenye afya, elimu ya afya inayojenga ujuzi na huduma za lishe na afya shuleni.
Hii ina maana kwamba elimu ya magonjwa yasiyoambukiza haipaswi kuwa somo la kusubiri mtu awe mgonjwa.
Mtoto anaweza kufundishwa mapema kwa nini ni muhimu kula mlo wenye uwiano, kwa nini mazoezi ni muhimu, madhara ya kutumia kupita kiasi vinywaji vyenye sukari, tumbaku na pombe, pamoja na umuhimu wa kudhibiti uzito na kufanya vipimo vya afya inapohitajika.
Utafiti uliofanywa Mwanza na Mtafiti, Evangelista Malindisa na wenzake uliowahusisha vijana 245 wenye umri wa miaka 18 hadi 34, ulibaini kuwa asilimia 7.8 walikuwa na kisukari, huku asilimia 15.5 wakiwa na hali ya kutovumilia sukari vizuri.
Utafiti huo pia ulibaini kuwa asilimia 45.1 walikuwa na matatizo ya mafuta kwenye damu, asilimia 34.3 walikuwa na shinikizo la damu na asilimia 11.8 walikuwa na unene wa tumbo.
Takwimu hizi hazimaanishi kwamba kila mtoto au kijana ataishia kuwa na kisukari au ugonjwa wa moyo. Lakini zinaonyesha kuwa vihatarishi vya magonjwa haya vinaweza kuonekana mapema, hivyo kinga nayo inapaswa kuanza mapema.
Kwa upande wa kisukari pekee, WHO inasema idadi ya watu wanaoishi na ugonjwa huo duniani iliongezeka kutoka milioni 200 mwaka 1990 hadi milioni 830 mwaka 2022.
Shirika hilo pia linasema lishe bora, mazoezi ya mara kwa mara, kudumisha uzito unaofaa na kutotumia tumbaku vinaweza kusaidia kuzuia au kuchelewesha kisukari aina ya pili.
Hivyo, kama tunataka kupunguza mzigo wa kisukari katika miaka ijayo, hatupaswi kusubiri mpaka mtu awe na miaka 40 au 50 ndipo tuanze kumfundisha namna ya kujikinga.
Lakini elimu ya afya isiishie kwenye mwanafunzi kukariri kwamba mboga ni nzuri au sukari nyingi ni mbaya, inapaswa kumjengea uwezo wa kufanya uamuzi.
Kwa mfano, mwanafunzi anaweza kufundishwa kutambua tofauti kati ya mlo wenye uwiano na mlo unaotawaliwa na kundi moja la chakula, kuelewa umuhimu wa kushughulisha mwili, kutambua madhara ya vinywaji vyenye sukari nyingi na kuelewa namna mazingira ya familia na jamii yanavyoweza kuathiri uchaguzi wa chakula.
WHO tayari ina mwongozo maalumu wa elimu ya ujuzi wa maisha shuleni kuhusu kinga ya magonjwa yasiyoambukiza. Mwongozo huo unasisitiza kushughulikia vihatarishi kama matumizi ya tumbaku, lishe isiyofaa na kutofanya mazoezi kupitia elimu ya afya na ujuzi wa maisha.
Wazazi, shule, wataalamu wa afya, Serikali na wadau wote wanapaswa kushirikiana. Shule inaweza kumfundisha mtoto kuhusu lishe bora, lakini ikiwa mazingira yanayomzunguka yanamsukuma kila siku kwenye vyakula visivyo na uwiano na kutofanya mazoezi, elimu hiyo inaweza kutomsaidia inaweza kuwa na nguvu ndogo.
Ndiyo maana wadau wanapendekeza mtazamo mpana wa shule inayokuza afya, unaojumuisha sera za shule, mazingira ya kujifunzia, elimu ya afya, lishe na huduma za afya. Kwa Tanzania, huu unaweza kuwa uwekezaji wa muda mrefu katika afya ya Taifa.
Tukiwafundisha watoto leo kuhusu lishe, mazoezi na vihatarishi vya magonjwa yasiyoambukiza, tunakuwa tunajenga kizazi kinachoweza kufanya uamuzi bora zaidi kuhusu afya yake, kwani magonjwa hayo hayapaswi kuwa somo linalofundishwa baada ya mtu kuugua. Elimu yake ianzie shuleni kwa sababu kinga inaanza kabla ya ugonjwa.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Songwe waanza mpango wa kutokomeza utoro shuleni | 0 | 4.68 | 27-08-2026 |
| 2 | Afya bora uzeeni inaanzia kwenye ujana | 0 | 6.82 | 28-08-2026 |
| 3 | Ukweli kuhusu maziwa kwenye matibabu | 0 | 6.66 | 28-08-2026 |
| 4 | Sillo azitaka taasisi za elimu kuandaa vijana kwa soko la ajira | 0 | 5.92 | 25-08-2026 |
| 5 | Міністэрства адукацыі зацьвердзіла праграму новага факультатыву для школаў | 0 | 10 | 04-08-2026 |
| 6 | В ВОЗ призвали к очному обучению школьников в новом учебном году | 0 | 0 | 30-08-2021 |
| 7 | В якутских школах в первые две недели учебного года будут дежурить врачи | 0 | 0 | 12-08-2020 |
| 8 | В российских школах смогут временно приостанавливать занятия из-за роста заболеваемости | 0 | 12.76 | 05-08-2026 |
| 9 | Минпросвещения будет вводить удаленку в школах только при всплесках заболеваемости ковидом | 0 | 0 | 26-01-2022 |
| 10 | Школам дали рекомендации на случай подъема заболеваемости ОРВИ и COVID-19 | 0 | 9.9 | 28-07-2026 |