Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Afya bora uzeeni inaanzia kwenye ujana

Дата публикации: 28-08-2026 10:35:56

Ulishawahi kufikiria, wewe kijana, namna bora ya kutunza afya yako ili uje kuwa na afya njema uzeeni?

Основное содержимое страницы с новостью.

By  Hadija Jumanne

Mwandishi wa Habari

Mwananchi

Muktasari:
  • Wataalamu wa afya na tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa baadhi ya tabia za vijana zinaweza kuathiri afya yao baadaye bila wao kutambua.

Dar es Salaam. Ulishawahi kufikiria, wewe kijana, namna bora ya kutunza afya yako ili uje kuwa na afya njema uzeeni?

Kama bado, hujachelewa. Afya bora ya uzeeni huanza kujengwa tangu ujana kupitia maamuzi madogo yanayofanywa kila siku.

Wataalamu wa afya na tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa baadhi ya tabia za vijana zinaweza kuathiri afya yao baadaye bila wao kutambua.

Miongoni mwa tabia hizo ni kula mara kwa mara vyakula vyenye mafuta na chumvi nyingi kama chipsi, mihogo ya kukaanga na sambusa; kutumia sukari nyingi kupitia vinywaji baridi na vitafunwa kama keki, ice cream na biskuti; kuruka milo, hasa kifungua kinywa; pamoja na kunywa maji kidogo.

Kwa kutambua umuhimu wa kujenga afya mapema, Mwananchi ilizungumza na Ofisa lishe mtafiti kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Fatma Juma, ambaye anaeleza mambo muhimu ambayo vijana wanapaswa kuyazingatia ili kuwa na afya njema hadi uzeeni.

Juma anasema lishe sahihi ni nguzo muhimu ya afya ya muda mrefu. Mwili unahitaji mchanganyiko wa virutubisho ili kujenga mwili, kutoa nguvu na kuulinda dhidi ya magonjwa.

Anasema mlo kamili unapaswa kujumuisha makundi sita ya vyakula. Makundi hayo ni nafaka, mizizi na ndizi za kupikwa; vyakula vinavyotokana na wanyama kama dagaa, maziwa, nyama na mayai; jamii ya kunde, karanga na mbegu kama maharage, njugu, dengu, mbegu za maboga na korosho.

Makundi mengine ni mboga za majani na mboga nyingine kama mchicha, matembele, bilinganya na mchunga; matunda kama maembe, mapera, mabungo na ukwaju; pamoja na mafuta salama.

“Vyakula hivi vina virutubisho vinavyosaidia kuupa mwili nguvu, kujenga na kukarabati mwili, kuulinda dhidi ya magonjwa, kuimarisha mifupa na meno, kuboresha uwezo wa kuona na kuongeza damu,” anasema.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, kijana anayejenga tabia ya kula mlo kamili kila siku huweka msingi wa kuzuia magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari, shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.

Makosa yanayofanywa na vijana

Juma anasema vijana wengi hufanya makosa ya lishe yanayoweza kuathiri afya yao baadaye. Kula vyakula vyenye mafuta na chumvi nyingi mara kwa mara, kutumia sukari kupita kiasi, kuruka milo na kutokunywa maji ya kutosha ni miongoni mwa tabia hizo.

“Tabia hizi husababisha mwili kukosa virutubisho muhimu na kuongeza hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukiza. Lishe duni ya leo inaweza kuwa chanzo cha matatizo makubwa ya kiafya kesho,” anasema.

Juma anasisitiza umuhimu wa kunywa maji ya kutosha kwa kuwa husaidia kusafirisha virutubisho, kuondoa taka mwilini na kudumisha utendaji mzuri wa mwili.

“Namshauri kijana kunywa angalau lita moja na nusu hadi mbili za maji kwa siku. Kiasi hiki kinaweza kuongezeka kulingana na hali ya hewa, hasa wakati wa joto,” anasema.

Mbali na lishe, anasema mazoezi ni muhimu katika kujenga afya ya muda mrefu. Vijana wanashauriwa kufanya mazoezi kwa angalau dakika 30 kwa siku. Kukimbia, kuogelea, kuendesha baiskeli na mazoezi ya viungo ni miongoni mwa shughuli zinazoweza kufanyika. Pia, kutembea na kufanya kazi za nyumbani husaidia kuufanya mwili kuwa hai.

Afya ya akili nayo ni muhimu

Juma anasema usingizi wa kutosha huupa mwili muda wa kupumzika, kujirekebisha na kurejesha nguvu. Vijana pia wanapaswa kuepuka uvutaji sigara na matumizi ya pombe kupita kiasi.

“Afya ya akili pia ni sehemu muhimu. Msongo wa mawazo unaweza kuathiri afya ya mwili na mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, na hivyo kuchangia kuongezeka kwa uzito na hatari ya magonjwa yasiyoambukiza,” anasema.

Hatimaye, mtaalamu huyo anasema afya njema uzeeni si suala la bahati, bali ni matokeo ya maamuzi yanayofanywa leo. Kula vizuri, kufanya mazoezi, kunywa maji ya kutosha, kupata usingizi na kuepuka tabia hatarishi ni hatua muhimu za kuwekeza katika afya ya baadaye.

Kwa vijana, ujumbe ni mmoja: usisubiri uzee ndipo uanze kuitunza afya yako. Anza leo, kwa sababu afya ya kesho hujengwa na tabia za leo

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Tiba asili si uchawi, wananchi waelimishwa06.6627-08-2026
2Ukweli kuhusu maziwa kwenye matibabu 06.6628-08-2026
3Kuahirisha mambo kulivyo hatari kwa afya yako06.9425-08-2026
4Elimu ya magonjwa yasiyoambukiza ianzie shuleni06.0128-08-2026
5UCHAMBUZI WA MJEMA: Tusijidanganye, tunahitaji maandalizi haya kabla ya 2030018.3327-08-2026
6Раскрыта лучшая диета для поддержания здоровья01013-08-2026
7Utafiti wafichua uhusiano wa ulaji, VVU na hatari ya kisukari05.0628-08-2026
8Matumaini mapya kwa waliojifungua kwa upasuaji08.5225-08-2026
9Wakati sahihi wa kununua hisa ni huu06.4627-08-2026
10Ambulance kupunguza changamoto za rufaa Kibaha Vijijini05.2625-08-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 6.82. Источник: www.mwananchi.co.tz.