Utafiti mpya umeibua maswali kuhusu usalama wa muda mrefu wa ‘xylitol’ aina ya utamu inayopatikana katika peremende na bidhaa za usafi wa kinywa, baada ya kubaini uhusiano kati ya viwango vya juu vya dutu hiyo mwilini na ongezeko la hatari ya matukio makubwa ya moyo na mishipa.
Alhamisi, Agosti 27, 2026

Dar es Salaam. Utafiti mpya umeibua maswali kuhusu usalama wa muda mrefu wa ‘xylitol’ aina ya utamu inayopatikana katika peremende na bidhaa za usafi wa kinywa, baada ya kubaini uhusiano kati ya viwango vya juu vya dutu hiyo mwilini na ongezeko la hatari ya matukio makubwa ya moyo na mishipa.
Xylitol ni aina ya utamu unaotokana na kundi la kemikali linaloitwa alkoholi za sukari (polyols).
Kwa mujibu wa dailymail, utafiti huo umeangazia ‘xylitol’, aina ya utamu ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitumika kwenye peremende na bidhaa nyingine za vyakula na usafi wa kinywa.
Watafiti wamebaini kuwa watu wenye viwango vya juu vya xylitol kwenye damu walikuwa na hatari kubwa ya kupata matatizo makubwa ya moyo na mishipa.
Daktari bingwa mbobezi wa magonjwa ya ndani na kisukari, Profesa Kaushik Ramaiya amesema sukari ya viwandani ina kiwango cha juu kuliko sukari ya kawaida, hivyo vyakula hivyo vina madhara zaidi.
Kwa kawaida binadamu anatakiwa kula vijiko vitano vya sukari kwa siku, ila baadhi ya vyakula vina sukari iliyozidi mfano soda yenye ujazo wa mil350 ina sukari vijiko 10, juisi na vyakula vingine vya viwandani hali kadhalika,” amesema.
Pia amesema unywaji wa vinywaji vyenye sukari nyingi na mtindo wa maisha ni sababu ya ongezeko la wagonjwa wanaugua kisukari aina ya pili ‘Type 2 diabetes’.
Utafiti
Wanasayansi kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Charité, Berlin walichambua taarifa za washiriki 17,710 na kufuatilia uhusiano kati ya viwango vya xylitol na afya ya moyo kwa muda mrefu.
Katika ufuatiliaji wa miaka sita, watu waliokuwa na viwango vya juu vya xylitol walikuwa na asilimia 57 zaidi ya hatari ya kupata tukio kubwa la moyo na mishipa, ikilinganishwa na waliokuwa na viwango vya chini, baada ya kuzingatia sababu nyingine zinazojulikana kuongeza hatari, ikiwamo umri, jinsia, uvutaji sigara na shinikizo la damu.
Baada ya miaka 30, hatari ya mshtuko wa moyo, kiharusi au kifo kinachohusishwa na ugonjwa wa moyo ilikuwa juu kwa asilimia 18 miongoni mwa waliokuwa na viwango vya juu vya xylitol.
Mmoja wa watafiti, Dk Marco Witkowski amesema matokeo hayo yanaonyesha kuwa bado kuna mambo mengi yasiyojulikana kuhusu usalama wa muda mrefu wa baadhi ya vitamu vinavyotumiwa badala ya sukari.
Utafiti wa awali pia umependekeza kuwa xylitol kwa kiwango kikubwa inaweza kuongeza uwezekano wa damu kuwa nzito na kuganda kirahisi, jambo linaloweza kuchangia kutokea kwa mgando wa damu unaoweza kuziba mishipa.
Xylitol ni sukari aina ya alcohol inayopatikana kwa kiasi kidogo mwilini na pia huongezwa kwenye bidhaa mbalimbali kwa sababu ina utamu wenye kalori chache kuliko sukari. Pia imekuwa ikitumika katika bidhaa za meno kwa kuwa inaweza kusaidia kupunguza bakteria wanaosababisha kuoza kwa meno.
Hata hivyo, wataalamu ambao hawakushiriki utafiti huo wamesema matokeo haya hayatoshi kuthibitisha moja kwa moja kuwa xylitol husababisha mshtuko wa moyo au kiharusi, kwa kuwa utafiti uliangalia uhusiano kati ya viwango vya xylitol na matukio hayo.
Mjumbe wa Kamati ya Mawasiliano ya European Society of Cardiology, Profesa Dan Atar amesema matokeo yanaongeza umuhimu wa kufanya tafiti zaidi kuhusu usalama wa vitamu vinavyotumiwa kwa wingi katika jamii.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Utafiti wafichua uhusiano wa ulaji, VVU na hatari ya kisukari | 0 | 5.06 | 28-08-2026 |
| 2 | Ученые выявили новые риски искусственных подсластителей | 0 | 7 | 03-07-2026 |
| 3 | Учёные назвали главную опасность популярных сахарозаменителей | 0 | 5 | 21-07-2026 |
| 4 | Учёные назвали угрозу для здоровья от заменителя сахара | 0 | 5.97 | 01-08-2026 |
| 5 | Ученые расказали о неожиданной опасности заменителей сахара | -1 | 5 | 04-07-2026 |
| 6 | Ученые назвали восемь консервантов, которые могут быть опасны для сердца | 0 | 7 | 30-06-2026 |
| 7 | دراسة تحذر: المواد الحافظة تهدد القلب وترفع ضغط الدم | 0 | 7 | 21-05-2026 |
| 8 | Врач объяснил, действительно ли заменители сахара опасны для мозга | 0 | 11.77 | 04-08-2026 |
| 9 | Kuahirisha mambo kulivyo hatari kwa afya yako | 0 | 6.94 | 25-08-2026 |
| 10 | Кардиологи назвали 15 продуктов, которые опасны для здоровья сердца | 0 | 17.78 | 07-08-2026 |