Umewahi kufahamu tabia ya kuahirisha mambo si uvivu tu wa kawaida bali ni ishara ya mapambano ya kisaikolojia yanayoendelea ndani ya ubongo wako?
Dar es Salaam. Umewahi kufahamu tabia ya kuahirisha mambo si uvivu tu wa kawaida bali ni ishara ya mapambano ya kisaikolojia yanayoendelea ndani ya ubongo wako?
Utafiti mpya wa kisayansi (systematic review and meta-analysis) uliochapishwa hivi karibuni katika Jarida la Frontiers in Psychiatry, umefichua uhusiano wa moja kwa moja kati ya tabia ya kuahirisha mambo na matatizo ya afya ya akili, hususan sonona (depression), wasiwasi (anxiety) na msongo wa mawazo (stress).
Utafiti huo ulioratibiwa na jopo la wanasayansi wakiongozwa na Yuyang Nie wa Chuo Kikuu cha Beijing Normal nchini China, ulichambua tafiti 88 tofauti zilizohusisha jumla ya washiriki 63,323 kutoka nchi 17 duniani.
Matokeo ya utafiti huo yalileta tahadhari mpya kwa jamii kuhusu jinsi watu wanavyochukulia tabia ya kuahirisha mambo.
Kulingana na utafiti huo, kulibainika uhusiano wa hisia wa wazi kuhusu tabia ya kuahirisha mambo na hali ya mtu kuwa na sonona, wasiwasi na msongo wa mawazo kwa viwango tofauti tofauti.
Utafiti huo pia umegusa aina mpya ya kuahirisha mambo inayowatesa wengi hasa kuahirisha hadi muda wa kulala.
Tabia hii imehusishwa kwa karibu na uraibu wa simu za mkononi na matumizi ya kupitiliza ya vifaa vya kielektroniki kabla ya kulala.
Matokeo yake ni kupungua kwa ubora wa usingizi, jambo linaloharibu kabisa afya ya akili.
Watafiti hao wamebainisha, tabia ya kuahirisha mambo imeenea kwa kiwango kikubwa kuliko inavyodhaniwa, kwenye jamii ya kawaida, kati ya asilimia 20 na 25 ya watu wazima wanaishi na tabia hiyo.
Hali ni mbaya zaidi miongoni mwa vijana, hususan wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo hadi asilimia 70 wanajipambanua kama watu wenye tabia sugu ya kuahirisha mambo.
Ripoti hiyo inafafanua upo ‘mzunguko mbaya usioisha’ (vicious circle) unaowaweka watu katika kifungo cha kisaikolojia.
Akizungumzia utafiti huo, Mtaalamu wa Saikolojia, Ramadhan Masenga amesemna tabia ya watu kuahirisha mambo inatokana na ubongo kuwa shughuli nyingi katika eneo la hisia na hivyo mtu hushindwa kuwa makini kwa jambo moja analofanya.
“Mtu wa namna hiyo si anaahirisha mambo ya maana pekee, bali jambo lolote analofanya yeye huahirisha mnaweza kuzungumza anakuwa anachezea simu au kufanya jambo lingine.
“Watu wa aina hii hawana uwezo wa kutekeleza mambo yao maana akili yao inatafuta mambo mapya ya kuwapa furaha kwa kuwa muda wote wanawaza hatari,” amesema.
Anasema kwa mwenye tabia hiyo, hupendelea starehe zaidi na vitu vingi vya kumfurahisha.
"Mtu huyu hupenda zaidi kwenda maeneo yenye starehe na anapenda vitu vingi vya kumfurahisha," amesema.
“Jambo la kufanya kama una changamoto hii kwanza ni kufanya mazoezi ya yoga, kufanyiwa masaji kunasaidia mtu kurejesha hali yake ya kawaida,” amesema.
Masenga amesema wakati mwingine kutokana na tabia hiyo inayochochewa na mwili kuwa na taarifa ya hatari katika mazingira yasiyo ya hatari wakati mwingine kunachangia mtu kuwa na hasira muda wote.
“Mtu anaweza kukanyagwa kwenye daladala bahati mbaya lakini anakuwa na mkali sana licha ya kuombwa msamaha, hapo ni mwili wake una taarifa kuwa amedharauliwa kwa hiyo anapaswa kuchukua hatua,” amesema.
Mambo mengine yaliyosahauriwa kupitia utafiti huo ili kudhibiti hali hiyo katika hatua za awali ni shule na vyuo vikuu kuweka mifumo ya kuwabaini mapema na kuwasaidia kufuata mipango yao ya kila siku.
Vilevile madaktari na washauri wa kisaikolojia wanapaswa kutambua uhusiano huu na kutumia tiba ya tabia na utambuzi (Cognitive Behavioral Therapy - CBT), inayounganishwa na sayansi ya neva ili kuwasaidia wagonjwa wao kujenga mbinu sahihi za kudhibiti hisia.
“Kujifunza namna ya kukabili hisia hasi badala ya kuzikimbia ndio ufunguo mkuu wa kushinda tabia ya kuahirisha mambo na kulinda afya ya akili,” utafiti huo umeeleza.
Utafiti huo unaeleza kuwa hisia hasi kama wasiwasi, sonona, na msongo wa mawazo hudhoofisha motisha ya mtu, utendaji wake wa kazi na uwezo wa kujiamini.
Jambo hilo humfanya muhusika akimbilie kuahirisha majukumu yake kama njia ya kukwepa maumivu ya kisaikolojia kwa muda mfupi.
Changamoto ilivyo
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ya 2024 ilieleza 2022 Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Tanzania Mirembe kulikuwa na ongezeko la idadi ya wagonjwa waliopatiwa matibabu ya magonjwa ya akili kutoka wagonjwa 3,472 mwaka 2019 hadi 5,060 mwaka 2022, sawa na asilimia 31 ya wagonjwa.
Kwa mwaka 2020 mzigo wa maradhi ya akili umechangia kiwango cha vifo vya kujinyonga kwa asilimia 8.15 kwa kila watu 100,000.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Afya bora uzeeni inaanzia kwenye ujana | 0 | 6.82 | 28-08-2026 |
| 2 | UCHAMBUZI WA MJEMA: Tusijidanganye, tunahitaji maandalizi haya kabla ya 2030 | 0 | 18.33 | 27-08-2026 |
| 3 | Utamu wa peremende waibua tahadhari mpya afya ya moyo | 0 | 5.36 | 27-08-2026 |
| 4 | Uso unavyoweza kuonyesha dalili za figo kuanza kuathirika | 0 | 10 | 25-08-2026 |
| 5 | Wakati sahihi wa kununua hisa ni huu | 0 | 6.46 | 27-08-2026 |
| 6 | Врач предупредил о «тихих убийцах» здоровья мозга | 0 | 5 | 18-07-2026 |
| 7 | Как смартфон замечает, что вам плохо? Разбираемся в приложениях для психического здоровья | 0 | 0 | 05-10-2020 |
| 8 | Maofisa elimu, wakuu wa shule kikwazo utekelezaji elimu jumuishi -2 | -5 | 3 | 29-06-2026 |
| 9 | 39 Uncommon Addictions People Talked About In A Serious Thread | 0 | 16.64 | 23-07-2026 |
| 10 | ‘Wagonjwa wengi wa shinikizo la damu hawajitunzi' | 0 | 7 | 02-07-2026 |