Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Bunge lafuta Tasnia ya Pareto

Дата публикации: 28-08-2026 17:34:48

Bunge limepitisha Muswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Tasnia ya Pareto wa mwaka 2026, huku wabunge wakitaka Serikali kuongeza msukumo katika uzalishaji wa zao hilo kutokana na umuhimu wake kiuchumi.

Основное содержимое страницы с новостью.

Ijumaa, Agosti 28, 2026

Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo

By  Habel Chidawali

Mwandishi wa Habari

Mwananchi

Muktasari:
  • Taarifa zinaonyesha kuwa, Tanzania inashika nafasi ya pili kwa uzalishaji wa Pareto duniani ikitanguliwa na Australia huku nchi za Kenya na Ruanda nazo zikiwa moja wapo ya nchi hizo.

Dodoma. Bunge limepitisha Muswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Tasnia ya Pareto wa mwaka 2026, huku wabunge wakitaka Serikali kuongeza msukumo katika uzalishaji wa zao hilo kutokana na umuhimu wake kiuchumi.

Muswada huo unalenga kufuta Sheria Namba Moja ya mwaka 1997 iliyoanzisha Tasnia ya Pareto, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kupunguza gharama za uendeshaji kwa kuunganisha taasisi zinazotekeleza majukumu yanayofanana.

Akiwasilisha muswada huo bungeni jijini Dodoma leo Ijumaa, Agosti 28, 2026, Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo amesema hatua hiyo inalenga kupunguza wingi wa taasisi za udhibiti zinazotekeleza majukumu yanayofanana, kuimarisha uratibu na kuongeza ufanisi katika matumizi ya rasilimali za umma.

Chongolo amesema muswada huo unaweka masharti kuhusu kufutwa kwa Sheria ya Tasnia ya Pareto pamoja na masuala ya mpito, ikiwemo kuhamisha majukumu, mali, madeni na watumishi wa Bodi ya Pareto kwenda Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA).

“Lengo la kufuta Bodi ya Pareto ni kupunguza wingi wa taasisi za udhibiti kwa shughuli zinazofanana, kuimarisha uratibu, kuboresha usimamizi wa udhibiti na kuhakikisha matumizi yenye tija ya rasilimali za umma katika sekta ya kilimo,” amesema Chongolo.

Kamati yataka kurugenzi

Katika maoni yake, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, imependekeza kuanzishwa kwa kurugenzi inayojitegemea ndani ya COPRA itakayokuwa na jukumu la kuratibu uzalishaji, ubora, masoko na maendeleo ya mnyororo wa thamani wa zao la pareto.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Deodatus Mwanyika amesema pendekezo hilo limetokana na umuhimu wa zao hilo kwa Tanzania, likizingatiwa kuwa ni zao la kipekee na la kimkakati kutokana na mchango wake katika uchumi na nafasi ambayo Tanzania inashikilia katika uzalishaji wa pareto duniani.

Tanzania inashika nafasi ya pili duniani kwa uzalishaji wa zao hilo.

“Serikali ihakikishe inalinda na kuhifadhi maslahi ya watumishi waliokuwa wa Bodi ya Pareto ambao wataendelea na ajira zao chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko na kwamba haki hiyo izingatie haki na stahili zao za msingi za kiutumishi,” amesema Mwanyika.

Kamati hiyo pia imeitaka Serikali kutoa elimu na uelewa wa kutosha kwa wadau na walengwa kuhusu mabadiliko hayo ya sheria, hususan kuhusu kufutwa kwa Bodi ya Pareto na kuhamishiwa kwa majukumu yake COPRA.

Mbunge wa Kilolo, Rita Kabati, amesema zao la pareto limekuwa na mchango mkubwa katika Taifa, lakini halijapewa thamani inayostahili, akiiomba Serikali kulitazama kwa karibu.

Kwa mujibu wa Kabati, licha ya Tanzania kushika nafasi ya pili duniani kwa uzalishaji wa pareto, zao hilo linalimwa na wakulima takribani 12,000 pekee nchini na linazalishwa katika eneo la ekari 13,000.

Amesema hali hiyo inaonyesha umuhimu wa Serikali kuweka mikakati ya kuongeza idadi ya wakulima na uzalishaji wa zao hilo ili kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa.

Naye Mbunge wa Bahi, Keneth Nollo amesema pareto ikipewa kipaumbele kama ilivyo kwa mazao mengine ya kimkakati, inaweza kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Tanzania.

Amesema kuna maeneo mbalimbali nchini yenye mazingira yanayofaa kwa kilimo cha pareto, hivyo Serikali inapaswa kuweka mazingira yatakayowezesha wakulima wengi zaidi kulima zao hilo.

Kwa mujibu wa wabunge hao, kuongeza uzalishaji wa pareto kutasaidia Tanzania kutumia vizuri fursa iliyopo katika soko la zao hilo na kuongeza kipato kwa wakulima pamoja na mapato ya Taifa.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Bwawa la Nyerere kufungua zaidi fursa kuvutia uwekezaji06.4927-08-2026
2UCHAMBUZI WA MJEMA: Tusijidanganye, tunahitaji maandalizi haya kabla ya 2030018.3327-08-2026
3Songwe waanza mpango wa kutokomeza utoro shuleni04.6827-08-2026
4MBEGU YA UCHUMI: Kugeuza umeme wa ziada kuwa fursa ya kiuchumi      07.327-08-2026
5Sillo azitaka taasisi za elimu kuandaa vijana kwa soko la ajira05.9225-08-2026
6Решения, принятые на заседании Правительства 28 мая 2026 года0030-05-2026
7Tech Sector Is Engine of Future Growth09.814-08-2026
8Решения, принятые на заседании Правительства 6 мая 2026 года0007-05-2026
9Документы к заседанию Думы 04 июня 2026 года01528-05-2026
10На нацпроект по экпорту в 2026 году направят дополнительные 24,76 млрд рублей0017-12-2025

Классификация: Экономика. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 7.71. Источник: www.mwananchi.co.tz.