Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Dolly Parton alikuwa na mawigi 350

Дата публикации: 28-08-2026 07:59:48

Maneno mengi yanaweza kutumika kumuelezea gwiji wa muziki wa Country, Dolly Parton, lakini neno “wa kawaida” si mojawapo.

Основное содержимое страницы с новостью.

By  Mwandishi Wetu

Mwananchi Digital

Mwananchi

Muktasari:
  • Kuanzia kwenye majalada ya albamu zake hadi kwenye zulia jekundu, mwimbaji huyo alijulikana kwa mtindo wake wa kuvutia na wa kupindukia uliokuwa na mapambo ya kung’aa, vitambaa vinavyoning’inia, nywele za bandia za kimanjano zilizoinuka juu na mavazi ya jukwaani yaliyobana mwili na kupambwa kwa vito.

Marekani. Maneno mengi yanaweza kutumika kumuelezea gwiji wa muziki wa Country, Dolly Parton, lakini neno “wa kawaida” si mojawapo.

Kuanzia kwenye majalada ya albamu zake hadi kwenye zulia jekundu, mwimbaji huyo alijulikana kwa mtindo wake wa kuvutia na wa kupindukia uliokuwa na mapambo ya kung’aa, vitambaa vinavyoning’inia, nywele za bandia za kimanjano zilizoinuka juu na mavazi ya jukwaani yaliyobana mwili na kupambwa kwa vito.

Jumanne wiki hii, ilitangazwa kuwa Dolly Parton amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80. Kifo chake kilithibitishwa kupitia video iliyowekwa Instagram na mpwa wake, Brian Seaver.

Katika kipindi cha takriban miaka 60 ya kazi yake, Parton alikuwa bila shaka msanii mkubwa wa kurekodi, mtunzi mahiri wa nyimbo, mfadhili na msimulizi wa hadithi mwenye kipaji.

Pia hakuna ubishi alikuwa nembo ya mitindo.

“Ni uchaguzi wangu. Sipendi kuwa kama kila mtu mwingine,” aliwahi kusema ali-pokuwa akitetea mtindo wake maarufu wa mavazi. “Kamwe singeshuka kiasi cha kuwa mtu wa kufuata mitindo; hilo ndilo jambo rahisi zaidi kufanya.”

Inaripotiwa kuwa Dolly alikuwa na zaidi ya wigi 350, zaidi ya jozi 2,000 za viatu, pamoja na jumba lenye ukubwa wa takriban futi za mraba 50,000 lililotumika kuhifadhi mavazi yake ya jukwaani yaliyopambwa kwa vito na mapambo mbalimbali.

Alikuwa na mavazi mengi kiasi kwamba aliandika kitabu kizima kuhusu mitindo yake, kinachoitwa Behind the Seams: My Life in Rhinestones.

Pia aliimba kuhusu mtindo wake katika nyimbo zake, kuanzia wimbo wake wa mwaka 1967, Dumb Blonde, hadi Backwoods Barbie wa mwaka 2008.

Mtindo wake haukuwavutia mashabiki pekee, bali pia uliwaathiri wasanii wengine wa muziki wa country, akiwemo Miley Cyrus, Kacey Musgraves na Carrie Underwood, ambao wote waliwahi kuonekana katika vipindi vyao vya kuvaa mitindo yenye mapambo ya kung’aa na sura ya “cowgirl”.

Aidha, Dolly aliwahi kushirikiana na Emma Grede na Khloé Kardashian wa kampuni ya Good American katika mkusanyiko wa mavazi ya Denim na mavazi mengine uitwao Joleans.

Kama alivyoimba katika albamu yake ya kwanza: “Huyu mrembo si mjinga wa mtu yeyote.”

Mwanzo wa mtindo wake wa kipekee

Msingi wa mtindo wa Dolly wa mavazi ya kuvutia na yenye ladha ya Magharibi ulianza muda mfupi baada ya kuhamia Nashville mwaka 1964, akiwa na umri wa miaka 18, akiwa na lengo la kuanza rasmi safari yake ya muziki.

Hata hivyo, baba yake na babu yake hawakupendezwa na mtindo huo, na katika siku zake za mwanzo aliadhibiwa kwa sababu ya mwonekano wake.

Katika kitabu chake cha mwaka 2023, Behind the Seams: My Life in Rhinestones, Dol-ly aliandika kwamba mwonekano wake ulikuwa suala kubwa mwanzoni mwa kazi yake.

Alipopata mkataba wake wa kwanza wa kurekodi, Fred Foster, aliyekuwa mkuu wa Monument Records, alitaka sana kubadilisha mtindo wake na kumpa muonekano wa muziki wa pop wa miaka ya 1960.

Dolly aliandika kwamba walitaka anyooshe nywele zake, aonekane mwenye “mtindo zaidi” na avae mavazi yasiyokuwa na mapambo mengi. Lakini yeye hakupendezwa kabisa na wazo hilo.

Amesema alihisi kama amevuliwa utambulisho wake na kwamba hangeweza kufanya kazi yake vizuri kama msanii ikiwa hangejisikia kuwa yeye mwenyewe.

Wakati huo, si Foster pekee aliyemkosoa. Wengine walimwambia kwamba alionekana zaidi kama mtu tofauti kuliko mwimbaji.

Lakini Dolly alijibu kwa kujiamini kwamba alikuwa na mawazo mazuri na ubunifu, na kwamba alikuwa na kitu kikubwa zaidi cha kuuza kuliko mwonekano wake pekee.

Hollywood na mapambo yasiyo na mwisho

Baadaye Hollywood ilimkaribisha, naye akaingia kwa nguvu. Alishinda Tuzo ya Grammy kwa wimbo wake Here You Come Again na akaigiza katika filamu kadhaa zilizofanikiwa, hatimaye akipata nyota kwenye Hollywood Walk of Fame mwaka 1984.

Kwa miaka iliyofuata, Dolly aliendelea kujaribu mitindo mbalimbali ya mawigi, viatu virefu na mapambo mengi ya kung’aa.

Alipendelea rangi zinazong’aa, mavazi yaliyobana mwili na mara nyingi alionekana akiwa na kucha ndefu  pamoja na vipodozi vilivyopambwa kikamilifu.

Mavazi yake yaliyopambwa kwa vito, pamoja na tabasamu lake kubwa, yalikuwa se-hemu ya mwonekano uliomfanya aonekane kila alipoingia.

“Usiache kuacha jiwe la kung’aa bila kuligeuza,” aliwahi kumwambia Andy Warhol katika mazungumzo yaliyofanywa kwa jarida la Interview.

Mtindo huo wa kupindukia uliambatana na kujitambua kwake. Dolly mara nyingi alitu-mia ucheshi kujitania kuhusu mwonekano wake, jambo lililomsaidia kuwanyamazisha wakosoaji na wakati huohuo kudhibiti kabisa taswira yake hadharani.

Katika filamu The Best Little Whorehouse in Texas ya mwaka 1982, aliwahi kusema:

“Inagharimu pesa nyingi kuonekana wa gharama nafuu hivi.”

Pengine hilo ndilo lililofanya Dolly Parton kuwa zaidi ya mwimbaji alikuwa alama ya utamaduni na ikoni ya mitindo ambaye aliunda kanuni zake mwenyewe.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Vifo vya mastaa walioenziwa kwa bendera nusu mlingoti07.7226-08-2026
2Dolly Parton streams skyrocket after her death, making her the most streamed artist globally06.3128-08-2026
3Dolly Parton's cause of death is revealed011.8826-08-2026
4Dolly Parton skips Dollywood event over health concerns07.8314-08-2026
5Dolly Parton skips Dollywood event over health concerns07.8314-08-2026
6Koffi Olomide ana historia ndefu Tanzania08.2628-08-2026
726.08.2026 – Langsam Gesprochene Nachrichten011.0726-08-2026
8Kinachofuata kwa Dk Nchimbi01027-08-2026
9Ndejembi awakuna wadau, apewa angalizo01027-08-2026
10Mapato Stendi ya Magufuli yapaa01027-08-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 10.42. Источник: www.mwananchi.co.tz.