Soma hapa...
Manchester City imekutwa na hatia ya makosa 114 kati ya 115 ya uvunjaji wa kanuni za fedha za Ligi Kuu England (EPL).
Mamlaka inayosimamia Ligi Kuu England iliituhumu klabu hiyo kwa kufanya udanganyifu katika masuala ya kifedha na utawala yaliyofanyika kwa nyakati tofauti kuanzia msimu wa 2009/2010 hadi mwaka 2023.
Kesi hiyo ilianza kusikilizwa na jopo huru ambalo lilihitimisha usikilizaji wake mwaka 2024.
Tangu wakati huo, kumekuwa na muda mrefu wa kusubiria majibu ya uamuzi huo jambo ambalo lilianza kukatisha tamaa watu wengi ambao wana shauku ya kuona hukumu ya mashtaka hayo.
Na imefichuka kwamba tayari jopo linaloshughulikia jambo hilo limeshamaliza kazi yake na klabu zimeshajulishwa kuhusu uamuzi huo.
Kukutwa na hatia katika mashtaka hayo kunaweza kupelekea adhabu nzito kwa Manchester City ambazo zinaweza kuiathiri ushiriki wake kwenye Ligi Kuu England (EPL).
Miongoni mwa adhabu hizo ni kukatwa pointi jambo linaloweza kuifanya inyang’anywe mataji ya EPL ambayo ilitwaa katika misimu husika.
Inaripotiwa kwamba Manchester City inajipanga kukata rufaa juu ya uamuzi huo.
Msemaji wa Manchester City, amesema kwamba klabu hiyo inasubiria uamuzi wa bodi inayoshughulikia suala hilo.
“Mchakato wa Ligi Kuu unaendelea ukiwa na viashiria vya kumalizika na suala lina usiri mkubwa. Nafasi ya Manchester City inabakia kuwa ileile kama ya taarifa ya klabu ya Februari 2023,” amesema Msemaji huyo.
Mara zote, Manchester City imekuwa ikikanusha kuwa na hatia ya makosa hayo ambayo inatuhumiwa kuyafanya ndani ya miaka 14.
Awali ilishtakiwa kwa makosa 130 lakini yalipunguzwa hadi kubakia makosa 115.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Ureno yaanza kibabe Ligi ya Mataifa Ulaya | 0 | 10 | 25-09-2026 |
| 2 | Kanuni yazigharimu Yanga, Simba mamilioni | 0 | 10 | 25-09-2026 |
| 3 | Hii hapa sababu kukosa usingizi ukiwa na uchovu | 0 | 8.1 | 07-08-2026 |
| 4 | Shalulile apewa onyo kali Yanga | 0 | 10 | 24-09-2026 |
| 5 | Yanayowasubiri wahitimu mitaani | 0 | 0 | 20-07-2026 |
| 6 | Chanzo ghorofa kupigwa mnada kwa mkopo wa Sh10 milioni | 0 | 5 | 20-07-2026 |
| 7 | Malipo posho za madaktari pasua kichwa hospitalini | 0 | 10 | 20-09-2026 |
| 8 | Migogoro inapogeuka rafiki wa ndoa | 0 | 10 | 09-08-2026 |
| 9 | Ulaji, mazoezi silaha magonjwa yasiyoambukiza | 0 | 10 | 07-08-2026 |
| 10 | Manchester City found guilty of breaking Premier League’s financial fair play rules | 0 | 5.64 | 25-09-2026 |