Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Hii hapa sababu kukosa usingizi ukiwa na uchovu

Дата публикации: 07-08-2026 08:29:58

Soma hapa...

Основное содержимое страницы с новостью.

By  Mariam Mbwana

Mwananchi Comminications Ltd

Muktasari:
  • Usingizi ni moja ya mambo muhimu kwa maisha ya binadamu, ili kuifanya mifumo ya mwili kufanya kazi vizuri.

Dar es Salaam. Ni usiku, mwili umechoka baada ya pilikapilika za kutwa nzima.

Unajilaza kitandani ukiamini usingizi utakuja mara moja, lakini saa zinayoyoma bila ya kupata lepe la usingizi, Unageuka kulia, kushoto hadi kunakucha bila ya kupata usingizi wa kutosha huku ukijihisi uchovu zaidi.

Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa hali hiyo inaweza kusababishwa na mambo mbalimbali yanayohusisha mtindo wa maisha, afya ya akili na mwili, pamoja na mazingira ya kulala.

Kwa mujibu wa makala iliyochapishwa katika tovuti ya afya ya healthline,  hali hiyo huweza kusababishwa na msongo wa mawazo, kulala mchana kwa muda mrefu, matumizi ya kafeini au hata matatizo ya kiafya yanayohusiana na usingizi.

Makala hiyo inabainisha msongo wa mawazo kama chanzo kikuu cha hali hiyo kutokea.

Kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni (WHO), msongo wa mawazo ni mvurugano katika akili,  kutokana sababu kadhaa kama vile mkwamo katika uhusiano, uchumi na mengineyo. Na huwakumba mtu mmoja kati ya wanne kwa nyakati tofauti.

Inaeleza kuwa akili iliyojaa mawazo na wasiwasi hufanya iwe vigumu kupata usingizi. Msongo wa mawazo ni moja ya sababu kuu zinazohusishwa na tatizo la kukosa usingizi.

Wataalamu wanaeleza kuwa hali ya wasiwasi huongeza umakini na tahadhari ya mwili, jambo linalofanya ubongo ushindwe kutulia wakati wa kulala.

Matumizi ya vinywaji vyenye kafeini

Kunywa kahawa, chai au vinywaji vingine vyenye kafeini karibu na muda wa kulala,  kunaweza kuathiri ubora wa usingizi.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali hata kiwango cha miligramu 200 za kafeini,  kinaweza kuendelea kuwa na athari mwilini kwa saa nyingi baada ya kunywewa.

Wataalamu wanashauri kuepuka matumizi ya kafeini angalau saa nne hadi sita kabla ya kwenda kulala.

Makala hiyo inaeleza kuwa mwanga wa buluu unaotolewa na simu, kompyuta, televisheni na tabiti hupunguza uzalishaji wa homoni ya melatonin, ambayo husaidia mwili kujiandaa kwa usingizi.

Kutokana na hali hiyo, wataalamu wanashauri kuacha kutumia vifaa hivyo angalau saa mbili kabla ya kulala.

Zingatia haya

Akizungumza na Mwananchi, mwanasaikolojia Modesta Kimonga, anasema  ili kuimarika kwa afya ya ubongo wa binadamu, mtu  anaitaji utulivu.

Anasema utulivu huo unapatikana kwa njia mbalimbali ikiwemo kupata muda wa kutosha wa kupumzika.

Anasema kuwa kitaalamu inashauriwa kulala kwa angalau saa saba  hadi nane  kwa mtu mzima

“Mtu anapopata muda wa kutosha kulala inausaidia ubongo kuboresha utendaji kazi wake,  ambao unasababisha hata viungo na mifumo mingine nayo kufanya kazi kwa ufanisi unaotakiwa, ”anaeleza na kuongeza:

“Kutofanya hivyo kunaweza kusababisha mhusika kuhatarisha afya yake ya ubongo na hatimaye kusababisha changamoto mbalimbali kujitokeza ikiwemo kumweka katika hatari ya kupata kiharusi, kupungua kwa uwezo wa kumbukumbu.’’

Kwa upande wake, Daktari kutoka hospitali ya Milembe, Dk Samweli Msigwa anasisitiza kuwa ili mtu aweze kulala vizuri ni muhimu kuzingatia kuacha kutumia simu, kompyuta na televisheni angalau dakika 30 hadi saa moja kabla ya kulala.

Pia kuepuka kahawa, chai, soda na vinywaji vyenye kafeini nyakati za jioni au muda mchache kabla ya kulala.

“Kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara na kuweka chumba cha kulala katika mazingira tulivu, safi, yenye hewa ya kutosha na mwanga hafifu,”anasema.

Iwapo unaendelea kuhisi uchovu kila siku na mbinu za kawaida za kuboresha usingizi hazikusaidii, ni muhimu kumwona daktari kwa uchunguzi zaidi.

Uchunguzi wa kitaalamu unaweza kubaini chanzo halisi cha tatizo na kusaidia kupata matibabu au ushauri utakaorejesha usingizi mzuri pamoja na nguvu za kufanya shughuli za kila siku.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Ijue siri ya kisukari iliyojificha kwenye wali, ugali01007-08-2026
2Ongezeko la wahitimu wa vyuo, wadau watoa pendekezo01010-08-2026
3Yanayowasubiri wahitimu mitaani0020-07-2026
4Hivi ndivyo mwanachuo anaweza kujiajiri01012-08-2026
5Wahadhiri vyuo vikuu watoa tamko kupinga kamatakamata0520-07-2026
6Ulaji, mazoezi silaha magonjwa yasiyoambukiza01007-08-2026
7Kukosana katika ndoa ni fursa kwa wenza, msinune01009-08-2026
8Migogoro inapogeuka rafiki wa ndoa01009-08-2026
9Chanzo ghorofa kupigwa mnada kwa mkopo wa Sh10 milioni0520-07-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 9. Тональность: 0. Информативность: 8.1. Источник: www.mwananchi.co.tz.