Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Zimbabwe yashangaza, DR Congo, Cameroon safi

Дата публикации: 25-09-2026 06:10:48

Soma hapa...

Основное содержимое страницы с новостью.

Ijumaa, Septemba 25, 2026

By  Mwandishi Wetu

Mwananchi Digital

Mwananchi

Muktasari:
  • Zimbabwe imepindua matokeo na kuifunga Sierra Leone mabao 3-2 baada ya kuwa nyuma kwa mabao mawili, huku DR Congo, Cameroon, Mauritania na Namibia zikianza kwa ushindi katika mechi za kuwania kufuzu AFCON 2027 zilizochezwa jana, Septemba 24.

Zimbabwe imepindua matokeo na kuifunga Sierra Leone mabao 3-2 baada ya kuwa nyuma kwa mabao mawili katika mechi ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 iliyochezwa jana, Septemba 24.

Sierra Leone ilianza kwa kasi na kufunga mabao mawili, lakini Zimbabwe ilirejea kwa nguvu na kupata mabao matatu yaliyoiwezesha kuibuka na ushindi huo.

Marshall Munetsi alifunga mabao mawili huku Tino Kadewere akifunga bao moja kwa Zimbabwe. Kwa upande wa Sierra Leone, Augustus Kargbo na Sullay Tarawallie ndio waliofunga mabao yao.

DR Congo yaanza kwa ushindi

DR Congo imeanza kampeni zake kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Guinea ya Ikweta.

Chancel Mbemba aliifungia DR Congo bao la kwanza katika dakika ya nne, kisha Yoane Wissa kuongeza la pili katika dakika ya 72.

Cameroon yaichapa Comoros

Cameroon imeanza vizuri baada ya kuifunga Comoros mabao 3-1.

David Nyingue alifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 39, huku Bryan Mbeumo akiongeza la pili katika dakika ya 48.

Comoros ilipata bao katika dakika ya 51 kupitia Warmed Omari, lakini Danny Namaso alifunga la tatu kwa Cameroon katika dakika ya 81.

Ivory Coast yaizamisha Ghana

Ivory Coast imeifunga Ghana mabao 2-0 katika mchezo mwingine wa kuvutia.

Malick Yalcouyé alifunga bao la kwanza katika dakika ya 44 kisha Franck Kessié kuongeza la pili kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 58.

Uganda yaikomalia  Tunisia

Uganda imeibana Tunisia na kutoka sare ya mabao 1-1 katika mchezo huo.

Adem Arous aliifungia Tunisia bao la kwanza katika dakika ya 12, lakini Uganda ilisawazisha katika dakika ya 68 kupitia Rogers Mato.

Mauritania, Namibia zaanza kwa ushindi

Mauritania imeanza kampeni kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Namibia yenyewe imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Congo ambalo limefungwa na Bethuel Muzeu katika dakika ya 47.

Libya, Botswana zatoka sare

Libya na Botswana zimetoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo mwingine wa kuwania kufuzu AFCON 2027.

Botswana ilianza vizuri na kufunga mabao mawili kupitia Tumisang Orebonye katika kipindi cha kwanza.

Libya ilirejea kipindi cha pili na kusawazisha kupitia Maruwan Al Hbeishi katika dakika ya 87 na Ezoo El Mariamy aliyepachika bao kwa mkwaju wa penalti katika dakika za nyongeza.

Matokeo ya mechi za kuwania kufuzu AFCON 2027 zilizochezwa Septemba 24, 2026

Zimbabwe 3-2 Sierra Leone

DR Congo 2-0 Guinea Ikweta

Cameroon 3-1 Comoros

Ivory Coast 2-0 Ghana

Tunisia 1-1 Uganda

Mauritania 3-1 Jamhuri ya Afrika ya Kati

Namibia 1-0 Congo

Libya 2-2 Botswana

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Kanuni yazigharimu Yanga, Simba mamilioni01025-09-2026
2Simba yamweka mtegoni Libasse01024-09-2026
3Shalulile apewa onyo kali Yanga01024-09-2026
4Ureno yaanza kibabe Ligi ya Mataifa Ulaya01025-09-2026
5Manchester City yakutwa na hatia EPL, yasubiri kiama01025-09-2026
6Simba yapiga mkwara ikiaga kwenda Sauzi01025-09-2026
7Taifa Stars yapoteza nyumbani, hesabu zahamia kwa Madagascar.01025-09-2026
8Southern African states push to keep mineral wealth at home09.3717-08-2026
9Патронный завод на Алтае рассматривает СНГ и Африку как альтернативу западным рынкам0020-12-2022
10Makonda: Rick Ross hajalipwa hata mia05.8824-09-2026

Классификация: Пресс-релизы. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 10. Источник: www.mwananchi.co.tz.