Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Hivi ndivyo mwanachuo anaweza kujiajiri

Дата публикации: 12-08-2026 10:19:40

Soma zaidi hapa...

Основное содержимое страницы с новостью.

Prime

Jumatano, Agosti 12, 2026

By  Elizabeth Edward

Mwandishi

Mwananchi

Muktasari:
  • Wasomi, wachumi wataja fursa za kidijitali, kilimo, ushauri wa kitaalamu, biashara na huduma wanazoweza kufanya wakiwa masomoni, wasisitiza kinachozidi kuhitajika si shahada pekee bali uwezo wa kuonesha kile mtu anachoweza kufanya

Dar es Salaam. Wakati kupata ajira baada ya kuhitimu chuo kikuu ikizidi kuwa changamoto kwa vijana wengi, wanafunzi wanashauriwa kutoutazama muda wa masomo kama kipindi cha kusubiri shahada pekee, bali fursa ya kujenga ujuzi, uzoefu na vyanzo vya kipato.

Wataalamu wa uchumi na elimu ya juu wanasema mwanafunzi anaweza kuanza shughuli ndogo inayolingana na taaluma yake au ujuzi alionao, huku akiendelea na masomo, jambo linaloweza kumsaidia kuingia katika soko la ajira akiwa tayari ana uzoefu na mtandao wa wateja.

Mtazamo huo unaendana na jitihada zinazoongezeka nchini za kuunganisha elimu ya juu na mahitaji ya soko la ajira mfano programu ya UDSM-Skilika ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inayolenga kuwapa wanafunzi ujuzi wa vitendo unaoongeza utayari wao wa kuingia katika ajira na ujasiriamali.

Pia, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) kina programu ya mafunzo ya vitendo ya uandishi wa mapendelezo ya miradi, ukuzaji mitaji na ujasiriamali kwa vijana na wahitimu wa vyuo.

Akizungumza na Mwananchi jana Jumanne, Agosti 11, 2026, Mhadhiri wa Uchumi, Gervas Katembo amesema changamoto kubwa kwa wanafunzi wengi ni kuamini ajira inaanza siku wanapopokea vyeti vyao.

Amesema chuo kinapaswa kuwa mazingira ya mwanafunzi kujenga uwezo wa kutatua matatizo ya jamii na kuyageuza fursa za kiuchumi.

“Mwanafunzi anatakiwa kuanza kujenga thamani yake akiwa chuoni. Anaweza kuanza kwa kazi ndogo, lakini akikusanya uzoefu, wateja na mtandao wa watu, anakuwa na msingi wa kujiajiri au kuajiriwa baada ya kuhitimu.

“Mwanafunzi anayekutana na tatizo la usafiri, chakula, malazi, biashara, elimu au huduma za kidijitali chuoni anaweza kulitazama kama changamoto inayoweza kugeuzwa kuwa wazo la biashara,” amesema Katembo.

Ameshauri mwanafunzi asichague shughuli kwa kuangalia fedha pekee, bali aangalie kama shughuli hiyo itampa ujuzi unaoweza kumsaidia baadaye na kumtengenezea fursa ya kupata kipato.

Shughuli hizo ni zipi

Huduma za kidijitali zinatajwa kuwa miongoni mwa maeneo yanayoweza kuchangamkiwa na wanafunzi wa kozi mbalimbali za teknolojia bila mtaji mkubwa.

Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Hafidh Mansoor amesema mwanafunzi anaweza kujifunza na kuuza huduma za kutengeneza tovuti, kubuni michoro ya matangazo, kusimamia kurasa za mitandao ya kijamii, kuhariri video, kupiga picha za bidhaa, kutengeneza maudhui na kufanya kazi za kutafsiri au kuandika.

Amesema mwanafunzi wa Tehama anaweza pia kutengeneza programu ndogo zinazotatua matatizo ya biashara au jamii, huku wanafunzi wa taaluma nyingine wakishirikiana nao katika masoko, fedha na usimamizi.

Mansoor amesema kwa sasa kinachozidi kuhitajika si shahada pekee bali uwezo wa kuonesha kile mtu anachoweza kufanya.

“Hivyo, mwanafunzi anayehitimu akiwa na portfolio ya kazi, wateja au mradi alioanzisha anaweza kuwa na faida zaidi kuliko anayemaliza akiwa na cheti pekee,”amesema Mansoor.

“Kwa wanafunzi wa elimu, biashara na masomo ya jamii, fursa zinaweza kupatikana katika ufundishaji wa ziada, utafiti, uandishi wa maudhui, uhariri, tafsiri, usimamizi wa biashara ndogo na utoaji wa huduma za kitaalamu.

“Mwanafunzi anayesoma uhasibu, kwa mfano, anaweza kujifunza kutoa huduma za kutunza kumbukumbu za fedha kwa wafanyabiashara wadogo, huku anayesoma masoko akisaidia biashara ndogo kutengeneza mikakati ya kutangaza bidhaa zao” amesema Katembo.

Mchumi huyo ameshauri pia wanafunzi kuanza biashara zinazolenga mahitaji ya wenzao chuoni, badala ya kuanza kwa kutafuta biashara kubwa.

Miongoni mwa shughuli hizo ni uuzaji wa vitabu na vifaa vya masomo, uchapishaji na uunganishaji wa nyaraka, chakula, nguo, vipodozi, vifaa vya simu, usafirishaji wa bidhaa na huduma za usafi.

“Mwanafunzi anaweza pia kuunda kikundi cha wanafunzi wenye ujuzi tofauti na kuanzisha biashara kwa pamoja. Kwa mfano, mwanafunzi wa biashara akashirikiana na wa Tehama na mawasiliano kuanzisha huduma ya kidijitali.

“Kwa wanafunzi wa lugha na mawasiliano, uandishi wa maudhui, uhariri, utangazaji wa kidijitali, usimamizi wa mitandao ya kijamii na huduma za mawasiliano ni maeneo yanayoweza kugeuzwa kuwa biashara,” amesema Katembo.

Mhadhiri wa OUT na mratibu wa programu ya uandishi wa miradi,  Dk Emmanuel Mallya amesema programu hiyo inafundisha  vijana na wanafunzi wa vyuo kuandika mawazo ya miradi ya biashara wanayoweza kuyatekeleza hata wakiwa wanaendelea na masomo.

“Kuna wanafunzi wanasoma na wameingia kwenye biashara ya bodaboda, sasa tunataka kuleta nidhamu kwa sababu tumegundua tatizo kubwa ni nidhamu ya fedha, inawezekana pesa anayokusanya kidogo kidogo kupitia biashara yake ya bodaboda anaweza kuwa na wazo la biashara kubwa zaidi.

“Tunachomsaidia ni kumfundisha kuandika wazo la mradi ili hata kama anahitaji uwekezaji kutoka kwa watu wengine basi awe na uwezo wa kuwashawishi kupitia andiko la kitaaluma,”amesema Dk Mallya.

Kilimo nacho ni fursa

Kwa wanafunzi wenye asili ya kilimo, mifugo, uvuvi au masomo yanayohusiana na chakula, wataalamu wanashauri kutazama kilimo kama biashara badala ya shughuli ya kawaida ya uzalishaji.

Mkurugenzi wa kampuni inayojihusisha na kilimo na ufugaji ya Mwanjfarm, Adrian Mwanji amesema wanafunzi wanaweza kuanza kwa uzalishaji mdogo wa mboga, kuku, mayai, uyoga, miche ya miti au bidhaa za chakula zinazoweza kusindikwa na kuuzwa.

“Wengine wanaweza kuingia katika biashara bila kumiliki shamba, kwa kuunganisha wakulima na wanunuzi, kusambaza pembejeo, kufanya masoko ya bidhaa za kilimo au kutumia teknolojia kuwasaidia wakulima kupata taarifa za masoko,” amesema Mwanji.

Hata hivyo, Mwanji anatahadharisha kuwa wanafunzi wasije wakafanya biashara kwa kiwango kinachohatarisha masomo yao.

“Muhimu kupanga ratiba, kutenganisha fedha za biashara na matumizi binafsi, kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi na kutumia sehemu ya faida kukuza biashara. Lengo si kila mwanafunzi kuwa mfanyabiashara mkubwa akiwa chuoni, bali kila mmoja kuhitimu akiwa na angalau ujuzi mmoja unaoweza kumuingizia kipato,” amesema.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Ongezeko la wahitimu wa vyuo, wadau watoa pendekezo01010-08-2026
2Wahadhiri vyuo vikuu watoa tamko kupinga kamatakamata0520-07-2026
3Hii hapa sababu kukosa usingizi ukiwa na uchovu08.107-08-2026
4Ijue siri ya kisukari iliyojificha kwenye wali, ugali01007-08-2026
5Yanayowasubiri wahitimu mitaani0020-07-2026
6Chanzo ghorofa kupigwa mnada kwa mkopo wa Sh10 milioni0520-07-2026
7Kukosana katika ndoa ni fursa kwa wenza, msinune01009-08-2026
8Migogoro inapogeuka rafiki wa ndoa01009-08-2026
9Ulaji, mazoezi silaha magonjwa yasiyoambukiza01007-08-2026
10Mashindano ya Feassa yafunga shule Morogoro Mjini, ikiibua sintofahamu01010-08-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 10. Источник: www.mwananchi.co.tz.