Wakulima wa mahindi nchini wametahadharishwa dhidi ya kutumia mbegu zisizothibitishwa ubora huku wakihimizwa kuhakikisha wanahakiki mbegu kabla ya kupanda ili kulinda uwekezaji wao na kuongeza nafasi ya kupata mavuno bora.
Morogoro. Wakulima wa mahindi nchini wametahadharishwa dhidi ya kutumia mbegu zisizothibitishwa ubora huku wakihimizwa kuhakikisha wanahakiki mbegu kabla ya kupanda ili kulinda uwekezaji wao na kuongeza nafasi ya kupata mavuno bora.
Tahadhari hiyo imetolewa leo Jumamosi, Agosti 28, 2026 na Mkurugenzi wa Kampuni ya uzalishaji wa mbegu na viuatilifu ya Bayer Tanzania, Sango Mwinyi, mkoani Morogoro wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya “DEKALB Mafanikio Shambani."
Kampeni hiyo inalenga kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kutumia mbegu halisi na suluhisho bora za kilimo.
Mwinyi amesema mabadiliko ya hali ya tabianchi yameendelea kuleta changamoto kubwa kwa wakulima wadogo, hali inayofanya upatikanaji wa mbegu zilizothibitishwa kuwa muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote.
Amesisitiza uamuzi wa kununua mbegu bila kuzihakiki unaweza kusababisha wakulima kupanda mbegu zisizo sahihi na hatimaye kupata mavuno duni.
Kwa mujibu wake, taarifa sahihi na uhakiki kabla ya kupanda ni hatua muhimu katika kujihakikishia tija shambani.
Kampeni hiyo inalenga kuwahamasisha wakulima kutumia aina tano za mbegu chotara za mahindi za DEKALB, ambazo zimebuniwa kuendana na mazingira mbalimbali ya kilimo nchini, ikiwemo maeneo yenye mvua chache.
Mbegu hizo, kwa mujibu wa kampuni hiyo, zinalenga kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambazo zimekuwa zikiathiri sekta ya kilimo.
Mbali na ujumbe wa kulinda uwekezaji wa mkulima, kampeni hiyo pia inakuja na promosheni yenye zawadi mbalimbali, zikiwemo simu janja, pikipiki, pampu za kunyunyizia, mashine za kupandia na kumenya mahindi. Mwisho wa kampeni hiyo, wakulima wawili wanatarajiwa kujishindia Toyota pick-up kila mmoja, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha ushiriki na matumizi ya mbegu bora.
Mkulima wa mkoani Kilosa, Morogoro, Juma Abdallah amesema kutumia mbegu zisizo sahihi zinaweza kukufanya ukapoteza nguvu na fedha kwa kuwa unapata mavuno kidogo.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Madiwani waitaka halmashauri ya wilaya Mufindi kulipa madeni | 0 | 5.02 | 28-08-2026 |
| 2 | Govt Seeks Urgent Measures On Cement Prices | 0 | 6.87 | 20-08-2026 |
| 3 | Warioba aeleza wasiwasi wake kupatikana Katiba mpya 2029 | 0 | 20 | 28-08-2026 |
| 4 | Производители выступили против предложенных Минсельхозом соглашений по ценам на удобрения | 0 | 0 | 17-03-2021 |
| 5 | Для КМНС предлагают ввести квоты на вылов рыбы для ведения хозяйственной деятельности | 0 | 0 | 10-12-2021 |
| 6 | Россия с 15 марта вводит экспортные пошлины на кукурузу и ячмень | 0 | 0 | 14-03-2021 |
| 7 | FPOs want to be treated like farmers, not corporates to get govt’s benefits | 0 | 7.35 | 17-07-2026 |
| 8 | На Кубани предлагают предоставлять субсидии научным сельхозучреждениям наравне с аграриями | 0 | 0 | 30-11-2021 |
| 9 | Аграриям уступили место в вагоне | 0 | 5 | 29-04-2026 |
| 10 | В Казахстане предложили ввести запрет на ввоз зерна автомобильным транспортом | 0 | 0 | 27-07-2022 |