Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Madiwani waitaka halmashauri ya wilaya Mufindi  kulipa madeni

Дата публикации: 28-08-2026 12:53:31

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, wameitaka halmashauri hiyo kuweka mikakati ya kuhakikisha madeni ya walimu na watumishi wa kada nyingine yanalipwa kwa wakati, ili kuwawezesha kufanya kazi kwa utulivu na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

Основное содержимое страницы с новостью.

Ijumaa, Agosti 28, 2026

Baadhi ya madiwani waliohudhuria baraza hilo wakisikiliza baada ya kuwasilisha  taarifa ya   hesabu za mwisho za halmashauri  kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

By  Mwandishi Wetu

Mwananchi Digital

Mwananchi

Muktasari:
  • Ushauri huo umetolewa leo Ijumaa, Agosti 28, 2026 na Diwani wa Mpanga Tazara, Flaviana Mpanda na Diwani wa Mtwango, Monte Kilamlaya, baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya hesabu za mwisho za halmashauri kwa mwaka wa fedha 2025/26.

Mufindi. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, wameitaka halmashauri hiyo kuweka mikakati ya kuhakikisha madeni ya walimu na watumishi wa kada nyingine yanalipwa kwa wakati, ili kuwawezesha kufanya kazi kwa utulivu na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

Ushauri huo umetolewa leo Ijumaa, Agosti 28, 2026 na Diwani wa Mpanga Tazara, Flaviana Mpanda na Diwani wa Mtwango, Monte Kilamlaya, baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya hesabu za mwisho za halmashauri kwa mwaka wa fedha 2025/26.

Taarifa hiyo iliwasilishwa katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.

Kilamlaya amesema halmashauri inapaswa kutafuta namna bora ya kulipa madeni hayo kwa wakati, ili kupunguza changamoto za kiuchumi zinazowakabili watumishi na kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa utulivu.

Amesema baadhi ya watumishi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za kifamilia na kiuchumi kutokana na madeni hayo, hali inayoweza kuathiri utendaji wao kazini.

“Halmashauri yetu hii ni kubwa, basi tuonyeshe ukubwa wetu. Tuhakikishe madeni haya yanalipwa kwa wakati ili walimu wawe na utulivu wakati wa kufundisha wanafunzi, kwani mwisho wa siku tunakuwa na matokeo mabaya. Vitu vingine tunasababisha sisi wenyewe kama halmashauri,” amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Castory Masangula amesema amepokea ushauri wa madiwani na kwamba baraza limeelekeza madeni ya watumishi wa kada mbalimbali, wakiwemo walimu, yalipwe.

Amesema kulipa madeni hayo kutasaidia watumishi kufanya kazi katika mazingira bora na kwa ari zaidi.

“Baraza limeshauri tulipe madeni haya ili watumishi hawa waweze kufanya kazi katika hali ya furaha, kwa sababu kama uchumi wako hauko vizuri huwezi kufanya kazi vizuri,” amesema Masangula.

Awali, akiwasilisha taarifa hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Fredrick Kibwana, amesema hadi kufikia Juni 30, 2026, halmashauri ilikuwa na madeni yenye thamani ya Sh1.6 bilioni.

Amesema madeni hayo hayahusiani na mishahara, bali yanajumuisha madai ya walimu ya Sh535 milioni, watumishi wasio walimu Sh488 milioni, wazabuni Sh629 milioni na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Sh21 milioni.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti Masangula amesema Baraza la Madiwani limeishauri halmashauri kuhakikisha fedha zinazotengwa kwa ajili ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura), zinatumika katika kutengeneza barabara za kimkakati.

Amesema hatua hiyo inalenga kuwawezesha wananchi kusafirisha mazao yao kabla ya kuanza kwa msimu wa mvua unaotarajiwa mwezi Oktoba.

Amesema halmashauri inakusanya ushuru kupitia barabara hizo, hivyo ni muhimu fedha zinazotengwa kwa ajili ya matengenezo zielekezwe kwenye maeneo yenye umuhimu mkubwa kiuchumi.

“Sisi kama halmashauri tunakusanya ushuru kupitia barabara hizi, hivyo kupitia fedha ambazo tunazitenga za asilimia 10 tunawapa Tarura ili kutengeneza barabara zetu za kimkakati, wananchi waweze kupitisha mazao yao mbalimbali kwenye barabara hizo,” amesema Masangula.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Wakulima waonywa kutumia mbegu zilizothibitishwa06.8728-08-2026
2KCMC yaitaka NIMR kuharakisha ‘One-Stop Centre’08.9628-08-2026
3Watenegenezaji, waingizaji dawa feki za asili kusakwa, NIMR kufungua kiwanda07.7128-08-2026
4Kilio cha abiria Stendi ya Magufuli chaanza kutatuliwa01028-08-2026
5Минобрнауки предложило заключать договоры целевого обучения со студентами для АЗРФ0009-06-2021
6В Магаданской области запустили ежегодную акцию «Собери ребенка в школу»09.2727-07-2026
7Минпросвещения планирует привлечь студентов к работе в школьных кружках0016-08-2019
8Магаданский промышленный техникум начал приемную кампанию для абитуриентов08.0111-06-2026
9Мишустин поручил повысить качество практикоориентированности программ в вузах0019-05-2025

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 9. Тональность: 0. Информативность: 5.02. Источник: www.mwananchi.co.tz.