Soma zaidi...
Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amechora ramani itakayoliwezesha Taifa kupata Katiba mpya mwaka 2029 ili Uchaguzi Mkuu wa 2030 uwe wa haki kuliko uliopita wa Oktoba 29, 2025.
Warioba amebainisha hayo leo Agosti 28, 2026 katika kongamano lililoandaliwa na wadau mbalimbali, wakiwamo Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), baada ya washiriki kujadili hali ya demokrasia, haki, ukweli, uwajibikaji na maridhiano ya kitaifa.
Kwa mujibu wa Jaji Warioba, kinachotakiwa ni kuwa na kitu cha mpito kwa kuchukua maeneo muhimu kadhaa yaliyopo katika Katiba, kisha kuyajadili kwa kuyatungia sheria, wakati mchakato wa Katiba mpya ukisubiriwa.

Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na mfumo wa uchaguzi, mgombea binafsi, mgawanyo wa madaraka, maadili na muungano, ambayo amesema yakifanyiwa kazi na kukamilika mwaka ujao kutakuwa na matumaini katika uchaguzi wa mwaka 2030.
“Tukiyakamilisha hayo, tunaweza kuwa na matumaini kwamba uchaguzi ujao 2030, utakuwa wa haki kuliko ulivyokuwa, la sivyo tutaendelea na utaratibu wa wagombea kuenguliwa,” amesema Warioba.
Jaji Warioba ameshauri kuwepo kwa utaratibu utakaowezesha Katiba kupitikana kabla ya mwaka 2030, badala ya kusubiri Tume ya Maridhiano na kamati zilizoundwa badala yake hatua zichukuliwe ili ifikapo mwaka 2027 Katiba ipatikane.
“Hili linataka utashi wa kisiasa wa viongozi wote na tujiandae kwa mwaka 2030,” amesema kiongozi huyo mstaafu.
Hata hivyo, Jaji Warioba ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, amesema kwa sasa haoni dalili za Taifa kupata Katiba mpya kabla ya mwaka 2029.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche akizungumza kwenye Kongamano la Kidemokrasia Tanzania liloandaliwa na Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) jijini Dar es Salaam leo Agost 28,2026, ambapo wadau mbalimbali wa masuala ya Sheria, Haki, Siasa na Katiba wamejumuika kujadiliana masuala ya kidemokrasia. Picha na Said Powa
Moja ya sababu aliyoitaja ni mlolongo mrefu wa kuufanikisha mchakato huo, unaochangiwa na Tume zilizoundwa na Serikali ikiwemo ya kubaini waliohusika na ghasia wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Tayari Tume hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wake, Jaji Shaaban Lila, imeanza kazi rasmi ikiwa na hadidu za rejea tano ikiwemo kuchunguza vifo visivyo vya kawaida vya watoto na makundi maalumu.
Jaji Warioba amesema kamati hiyo, ikimaliza muda wake italazimika kupata maoni ya wananchi ambayo huenda yakachukua takribani miezi sita, na si mwezi mmoja.
“Pia, kuna Tume ya Maridhiano ambayo haitafanya kazi kwa wiki chache au miezi michache. Kama tunataka kuwa na Tume ya Maridhiano, lazima ipewe muda wa kutosha, sioni kama unaweza kuipata ndani ya miezi michache.
“Sasa ukimaliza hiyo, unakwenda kwenye Katiba, mzungumze kwenye Katiba kisha ufuate utaratibu mliokubaliana. Mkishaipitisha iende kwenye kura za maoni na kisha kuwepo kwa kipindi cha mpito,” ameeleza Jaji Warioba.
Shivji na Katiba ya mpito
Hata hivyo, akichangia mada katika kongamano hilo, mwanazuoni mkongwe, Profesa Issa Shivji ameunga mkono hoja ya umuhimu wa kujenga mwafaka wa kitaifa, akisema Tanzania haina haja ya kukimbilia kupata Katiba mpya bila kwanza kuweka mazingira ya maridhiano.
Shivji amesema kutokana na ugumu wa kupata Katiba mpya kabla ya mwaka 2030, kuna haja ya kufikiria uwezekano wa kuwa na Katiba ya mpito kwa kurekebisha Katiba iliyopo.
Amependekeza maeneo manne ya kupewa kipaumbele katika hatua hiyo, likiwamo suala la Tume ya Uchaguzi.
Amesema badala ya kuishia kutumia jina “Tume Huru ya Uchaguzi”, kinachohitajika ni kurekebisha mfumo huo na kuwa na wajumbe wapya watakaokuwa na uwezo wa kusimamia uchaguzi kwa uhuru.
Pia, amependekeza kuundwa kwa Mahakama maalumu itakayoshughulikia mashtaka yanayohusu uwajibikaji wa watu watakaobainika kuhusika katika matukio ya kutekwa na kupotezwa kwa watu.
Wito wa kusimamia haki
Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi amewataka wadau kuendelea kutafakari na kusimamia misingi ya haki na maridhiano katika kutafuta suluhu ya changamoto zinazoikabili nchi.

Waziri Mkuu mstaafu JAJI Joseph Warioba akizungumza kwenye Kongamano la Kidemokrasia Tanzania liloandaliwa na Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), ambapo wadau mbalimbali wa masuala ya Sheria, Haki, Siasa na Katiba walijumuika kujadiliana. Picha na Said Powa
Mwabukusi amesema lengo la kongamano hilo ni kuwawezesha wadau kukaa pamoja na kutafakari hali ya nchi kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Naye, Profesa Anna Tibaijuka amegusia Katiba ya mwaka 1977 na kutaja maeneo ambayo anaona yanahitaji kufanyiwa mabadiliko ili kuboresha mfumo wa kisiasa na uchaguzi nchini.
“Tukiweza kufanya reforms (mabadiliko) ili mgombea uhuru aruhusiwe, kuwe na reform za uandikishaji wa vyama vya siasa, kuna sheria ambazo zinapingana na Katiba ya 1977, vyote hivyo vibadilike,” amesema.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Kilio cha abiria Stendi ya Magufuli chaanza kutatuliwa | 0 | 10 | 28-08-2026 |
| 2 | Mnyika ajitwisha dhamana mkutano Lissu aliodaiwa kufanya uhaini | 0 | 10 | 28-08-2026 |
| 3 | Serikali yataja sababu ya kuja na chanjo ya polio | 0 | 8.26 | 28-08-2026 |
| 4 | Bernameya Taybet bi Cama Cîhanê 2026 | 0 | 10.4 | 03-07-2026 |
| 5 | Lissu alivyohitimisha utetezi wake katikati ya mapingamizi ya Jamhuri | 0 | 8.26 | 28-08-2026 |
| 6 | CAG Kichere azishukia halmashauri tano Mara, atishia... | 0 | 6.09 | 28-08-2026 |
| 7 | Dk Nchimbi alivyopigwa chenga ya mwili | 0 | 10 | 28-08-2026 |
| 8 | Mazda Pushes CX-30 Redesign To 2031 | 0 | 23.5 | 20-08-2026 |
| 9 | Wakulima waonywa kutumia mbegu zilizothibitishwa | 0 | 6.87 | 28-08-2026 |
| 10 | Bernameya Taybet bi Cama Cîhanê 2026 | 0 | 12.6 | 16-06-2026 |