Soma hapa...
Dar es Salaam. Uongozi wa Kituo cha Mabasi cha Magufuli umeanza hatua za kutafuta suluhisho la kero ya ukosefu wa maeneo ya kupumzikia abiria katika sehemu ya chini ya kituo hicho.
Hatua hiyo imekuja wiki moja baada ya Mwananchi kuripoti kuhusu kero zinazowakabili abiria kutokana na ukosefu wa maeneo ya kukaa, hali inayowalazimu baadhi yao kukalia mizigo wakati wakisubiri usafiri.
Kwa sasa, abiria wanaotaka kufikia maeneo ya kupumzikia yaliyopo ndani ya kituo hicho hulazimika kupanda hadi ghorofa ya kwanza, jambo ambalo baadhi yao wamelieleza kuwa ni usumbufu, hasa wanapokuwa na mizigo.
Mbali na hilo, abiria wanaokwenda kupanda mabasi katika kituo hicho hulazimika kulipa Sh300 kama ada ya kuingia ndani ya kituo, jambo linaloongeza gharama za safari.
Kero hizo zimeongezeka kutokana na ongezeko la abiria tangu kuanza kutekelezwa kwa agizo la mabasi kuanzia na kumalizia safari zao katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli kuanzia Agosti 17, 2026.
Kinachoendelea
Maendeleo yaliyofanyika katika kituo hicho leo Ijumaa yameshuhudiwa na Mwananchi baada ya kukuta mafundi wakiendelea na ujenzi wa sehemu za kupumzikia abiria upande ambao mabasi yanayokwenda Kanda ya Kaskazini yanapaki.
Kabla ya kuanza kwa ujenzi huo, eneo hilo lilikuwa na uzio uliotenganisha sehemu ya maegesho ya mabasi ya Kanda ya Kaskazini na mabasi yanayokwenda mikoa mingine nchini.
Kutokana na mpango huo, mafundi wameanza kuondoa sehemu ya uzio na kuusogeza nyuma ili kupata nafasi ya kuweka viti vitakavyotumiwa na abiria wakati wakisubiri usafiri.
Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Kaimu Meneja wa kituo hicho, Naamini Leonard amekiri kufanyika kwa ujenzi huo na kusema ni sehemu ya jitihada za uongozi kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowasilishwa na abiria.
Baadhi ya abiria wamepongeza hatua hiyo wakisema ukosefu wa maeneo ya kukaa umekuwa ukiwalazimu kukaa sakafuni wakati wakisubiri usafiri, hali waliyoieleza kuwa si salama wala yenye faraja.
“Unakuta umefika na mizigo mingi, inabidi ukae tu hapa sakafuni ili kuepuka usumbufu, lakini kama uongozi wa stendi umeiona kero hii na kuchukua hatua, ni jambo la kushukuru,” amesema Nusura Khamis, mmoja wa abiria.
Naye Eliud Mweri amesema baadhi ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya abiria yamekuwa yakitumiwa na wafanyabiashara wadogo kuweka bidhaa zao.
Amehoji sababu ya wafanyabiashara hao kutumia maeneo hayo badala ya sehemu walizotengewa kwa ajili ya biashara.
“Hapa tulipaswa kukaa abiria, lakini ajabu kumejaa wafanyabiashara. Kama wametengewa maeneo yao, kwa nini wasikae huko? Kama ni kuja hapa, basi walete bidhaa chache kwa ajili ya kuwahudumia abiria badala ya kugeuza eneo hili kama maduka,” amesema Mweri.
Kwa upande wake, Arafa Gift mmoja wa wafanyabiashara katika jengo la abiria, amekiri kuwa baadhi ya abiria hawapendi kwenda katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kukaa, hali ambayo pia imekuwa ikiathiri biashara zao kwa sababu ya kukosa wateja.
Arafa ameshauri uongozi wa kituo hicho kuwasha lifti zilizopo katika jengo hilo ili kurahisisha abiria kufika ghorofani, akisema baadhi yao ni wazee, wagonjwa au wanaosafiri wakiwa na watoto.
Pia, ameshauri abiria wenye tiketi za safari wasilipishwe tena ada ya kuingia kituoni, akisema hatua hiyo itasaidia kupunguza gharama za usafiri kwa abiria.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Ijue siri ya kisukari iliyojificha kwenye wali, ugali | 0 | 10 | 07-08-2026 |
| 2 | Yanayowasubiri wahitimu mitaani | 0 | 0 | 20-07-2026 |
| 3 | Dk Nchimbi alivyopigwa chenga ya mwili | 0 | 10 | 28-08-2026 |
| 4 | Mnyika ajitwisha dhamana mkutano Lissu aliodaiwa kufanya uhaini | 0 | 10 | 28-08-2026 |
| 5 | Wahadhiri vyuo vikuu watoa tamko kupinga kamatakamata | 0 | 5 | 20-07-2026 |
| 6 | Migogoro inapogeuka rafiki wa ndoa | 0 | 10 | 09-08-2026 |
| 7 | Serikali yataja sababu ya kuja na chanjo ya polio | 0 | 8.26 | 28-08-2026 |
| 8 | Mfahamu Dk Nchimbi aliyejiuzulu makamu wa rais | 0 | 10 | 26-08-2026 |
| 9 | Lissu alivyohitimisha utetezi wake katikati ya mapingamizi ya Jamhuri | 0 | 8.26 | 28-08-2026 |
| 10 | Mashindano ya Feassa yafunga shule Morogoro Mjini, ikiibua sintofahamu | 0 | 10 | 10-08-2026 |