Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Makamua afichua kinachoendelea ndani ya Wakali Kwanza

Дата публикации: 26-08-2026 09:49:26

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Makamua amesema kundi la Wakali kwanza bado lipo na linaendelea na maandalizi ya kurejea katika anga la muziki baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, akisisitiza kuwa halijavunjika kama ambavyo baadhi ya watu wanavyodhani.

Основное содержимое страницы с новостью.

Jumatano, Agosti 26, 2026

Muktasari:
  • Akizungumza na Mwananchi, Makamua alisema safari yake ya muziki ilianza tangu akiwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Upanga, ambapo alianza kuimba nyimbo za kanisani kabla ya kuanza kuimba nyimbo za wasanii wa kimataifa. Hata hivyo, alisema msukumo wa kuimba kwa Kiswahili ulitokana na kuvutiwa na kazi za mwanamuziki Dully Sykes.

Dar es Salaam. Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Makamua amesema kundi la Wakali kwanza bado lipo na linaendelea na maandalizi ya kurejea katika anga la muziki baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, akisisitiza kuwa halijavunjika kama ambavyo baadhi ya watu wanavyodhani.

Akizungumza na Mwananchi, Makamua alisema safari yake ya muziki ilianza tangu akiwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Upanga, ambapo alianza kuimba nyimbo za kanisani kabla ya kuanza kuimba nyimbo za wasanii wa kimataifa. Hata hivyo, alisema msukumo wa kuimba kwa Kiswahili ulitokana na kuvutiwa na kazi za mwanamuziki Dully Sykes.

Alisema baada ya kupata hamasa hiyo aliingia studio na kurekodi nyimbo zake za kwanza akifanya kazi na maproduza Erico na Biz Man, kabla ya baadaye kufanya kazi na P Funk Majani. Wakati huo pia alishiriki mashindano mbalimbali ya muziki, ikiwemo Project Fame, ambapo alifanikiwa kushika nafasi ya nane na kupata fursa ya kwenda Afrika Kusini.

Baada ya safari hiyo, Makamua alisema aliungana na wasanii Joselini na Q Jay na mwaka 2000 wakaanzisha kundi la Wakali Kwanza. Lililojizolea umaarufu kupitia wimbo wao wa kwanza Wanatamani Niwe Chini Yao.

Alisema mafanikio ya kundi hilo yalitokana na mshikamano, nidhamu na kujituma kwa kila mwanachama, hali iliyowezesha kushinda tuzo mbalimbali na kutoa albamu zilizopokelewa vizuri na mashabiki.

"Wakali Kwanza haijafa na wala haitakufa kirahisi. Tulijenga jina hili kwa jasho letu na bado tuna mipango ya kuendelea kufanya kazi. Mashabiki wetu watulie, kuna mambo mazuri yanakuja," alisema Makamua.

Kuhusu ukimya wa kundi hilo kwa muda mrefu, alisema mabadiliko ya teknolojia yamebadili namna muziki unavyotengenezwa na kusambazwa, hivyo wameamua kuchukua muda kuhakikisha kazi watakazozitoa zitakuwa na ubora na zitadumu kwa muda mrefu kama nyimbo zao za zamani.

Msanii huyo alisema kwa sasa muziki wa R&B unapitia kipindi kigumu kutokana na kupungua kwa wasanii wanaoufanya. Lakini aliwapongeza wasanii wa Singeli kwa kuendelea kuuendeleza muziki huo ambao amesema umekuwa sehemu ya utambulisho wa Tanzania.

Akizungumzia tofauti kati ya kizazi chake na wasanii wa sasa, Makamua alisema maendeleo ya teknolojia ndiyo yameleta mabadiliko makubwa katika tasnia hiyo.

"Zamani hakukuwa na Instagram wala mitandao ya kijamii. Ili upate fedha ilibidi utoe nyimbo nzuri na upate maonesho. Ndiyo maana mpaka leo nyimbo nyingi za zamani bado zinaimbwa na zinapendwa," alisema.

Alisema ili muziki wa Tanzania uendelee kukua, kuna umuhimu kwa wasanii kukaa pamoja na Serikali na kuweka mikakati itakayosaidia kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo. Huku akisisitiza kuwa ushirikiano kati ya wasanii wakubwa na wadogo ni muhimu kwa maendeleo ya kizazi kipya cha wanamuziki.

Aidha, alisema wasanii wa Tanzania wanapaswa kujivunia utambulisho wao badala ya kuiga mitindo ya muziki kutoka nje, akieleza kuwa muziki wa Tanzania unaweza kufika kimataifa bila kupoteza asili yake.

Pia aliwataka wasanii kutumia vivutio vya utalii vilivyopo nchini katika utengenezaji wa video za nyimbo zao badala ya kutumia fedha nyingi kwenda kurekodia nje ya nchi.

"Tanzania ina maeneo mengi mazuri yenye mandhari ya kipekee. Tukiyatumia kwenye video zetu tutakuwa tunautangaza muziki wetu sambamba na kuitangaza nchi," alisema.

Makamua pia alizungumzia maadhimisho ya miaka 30 ya Bongo Fleva, akisema hakupokea mwaliko rasmi wa kushiriki katika tamasha hilo licha ya kuona taarifa kwenye mitandao ya kijamii zikimtaja miongoni mwa walioalikwa.

Alisema alishangazwa pia na namna baadhi ya wasanii waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Bongo Fleva, akiwemo Alikiba, wanavyokosa kutambuliwa ipasavyo katika baadhi ya matukio yanayohusu historia ya muziki huo.

"Sikupigiwa simu wala kupewa mwaliko rasmi. Niliona tu taarifa kwenye mitandao ya kijamii. Nitasubiri kuona kama nitaitwa kwenye maadhimisho yatakayofanyika mikoani," alisema.

Kuhusu suala la mirabaha, Makamua alisema hajawahi kunufaika na mfumo huo, akieleza kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa elimu kwa wasanii ili waelewe haki zao na namna mfumo wa mirabaha unavyofanya kazi.

Akitoa ushauri kwa wasanii chipukizi, alisema wanapaswa kuendelea kuamini ndoto zao, kufanya kazi kwa bidii, kuwa na nidhamu na kuheshimu taaluma yao, akisisitiza kuwa mafanikio katika muziki yanahitaji uvumilivu na kujituma.

"Nawapenda mashabiki wangu wote kwa kuendelea kunipa sapoti kwa miaka yote. Wao ndiyo sababu ya mimi kuendelea kufanya muziki," alisema.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Zuchu kama Fid Q tu!012.7828-08-2026
2Safari ya K Zungu hadi kutumbuiza Yanga06.8528-08-2026
3Koffi Olomide ana historia ndefu Tanzania08.2628-08-2026
4Mapato Stendi ya Magufuli yapaa01027-08-2026
5Hivi ndivyo Dk Nchimbi anavyoweza kurudi CCM01027-08-2026
6Jaji Warioba afichua alichozungumza na Dk Nchimbi kabla, baada ya kujiuzulu01027-08-2026
7Ndejembi awakuna wadau, apewa angalizo01027-08-2026
8Wakati sahihi wa kununua hisa ni huu06.4627-08-2026
9МакSим опубликовала первый пост в Instagram после выхода из комы0009-08-2021

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 9. Тональность: 0. Информативность: 6.27. Источник: www.mwananchi.co.tz.