Soma zaidi...
Prime
Alhamisi, Agosti 27, 2026

Dar es Salaam. Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amefunguka alichozungumza na Dk Emmanuel Nchimbi, saa chache baada ya taarifa yake ya kujiuzulu wadhifa wa Makamu wa Rais.
Sambamba na hayo, ameeleza walichozungumza walipokutana na Dk Nchimbi, kabla ya kujiuzulu kwake, akigusia masuala mbalimbali ya kitaifa.
Dk Nchimbi alimwandikia Rais Samia Suluhu Hassan, barua ya kuomba kujiuzulu Agosti 25, 2026 na saa chache baadaye, mkuu huyo wa nchi aliridhia ombi hilo.
Dk Nchimbi alimtembelea Jaji Warioba, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nyumbani Mbezi Juu, Dar es Salaam Julai 4, 2026.
Katika taarifa yake, aliyoisambaza kupitia kurasa za mitandao yake ya kijamii, Dk Nchimbi aliomba kujiuzulu kuanzia Septemba 4, 2026, wadhifa wa Makamu wa Rais.
Dk Nchimbi ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alitangaza uamuzi huo ikiwa ni siku 295 tangu alipoapishwa Novemba 3, 2025 kuwa Makamu wa Rais.
Baada ya kujiuzulu
Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi, Agosti 27, 2026 Jaji Warioba, ameeleza baada ya kuona taarifa ya kujiuzulu kwa Dk Nchimbi, aliwasiliana naye kwa simu kuthibitisha.
“Nilipoona taarifa nikampigia simu akanijulisha ni yake (taarifa ya kujiuzulu). Tukazungumza kama ameshapata uamuzi wa Rais,” amesema.
Amesema baadaye aliona taarifa kwamba Rais ameridhia ombi la Dk Nchimbi la kujiuzulu, alijaribu kumpigia simu Dk Nchimbi, lakini haikupokelewa.
“Nimekaa hadi jioni (Agosti 26, 2026) ndipo nikaona tamko la Katibu Mkuu kwamba chama kimemfukuza. Nikampigia simu haikupokelewa, nikapeleka ujumbe haukupokelewa,” amesema.
Kabla ya kujiuzulu
Jaji Warioba, amesema kabla ya hapo aliwahi kukutana na Dk Nchimbi akiwa Makamu wa Rais, walizungumza mambo mbalimbali ya kitaifa, ikiwemo umuhimu wa kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.
“Aliponitembelea hapa tulizungumza mengi, lakini mawili makubwa nilimshauri. Kwanza, matatizo tuliyonayo ni chachu kwamba hatujatengeneza Katiba Mpya. Kwa hiyo ushauri wangu kwa Serikali ni kwamba tuharakishe hili jambo tupate Katiba Mpya,” amesema.
Jana, Agosti 26, 2026 Katibu Mkuu wa CCM, Dk Asha-Rose Migiro, alitangaza taarifa ya kumfuta uanachama Dk Nchimbi, ikiwa ni maazimio yaliyofikiwa na kikao cha Kamati Kuu kilichoketi siku hiyo.
Wakati huohuo pia, Dk Migiro, alimtangaza Deogratius Ndejembi kuwa kada ambaye jina lake limependekezwa kuwa Makamu wa Rais, kumrithi Dk Nchimbi.
"Kufuatia hayo kwa kauli moja Kamati Kuu ya CCM, imepitisha ndugu Nchimbi afukuzwe uanachama kwa mujibu wa kanuni zetu.
Kwa hiyo tunapenda kuwafahamisha wanachama wote wa CCM na wananchi kwa ujumla kwamba CCM imefikia uamuzi huo na kuanzia hivi sasa ndugu Nchimbi amefukuzwa uanachama na sio mwanachama tena wa Chama cha Mapinduzi, pokeeni taarifa hiyo," alisema.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Kinachofuata kwa Dk Nchimbi | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 2 | Ndejembi awakuna wadau, apewa angalizo | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 3 | Hivi ndivyo Dk Nchimbi anavyoweza kurudi CCM | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 4 | Bunge kumthibitisha Ndejembi leo | 0 | 10 | 28-08-2026 |
| 5 | Utata ukomo umakamu wa rais wa Nchimbi, wanasheria watofautiana | 0 | 8.4 | 27-08-2026 |
| 6 | Migogoro inapogeuka rafiki wa ndoa | 0 | 10 | 09-08-2026 |
| 7 | Ijue siri ya kisukari iliyojificha kwenye wali, ugali | 0 | 10 | 07-08-2026 |
| 8 | Tamu, chungu kupigana busu kiafya | 0 | 0 | 02-07-2026 |
| 9 | Mbinu kukabili msongo wa mawazo kwenye familia | 0 | 5 | 06-07-2026 |
| 10 | Uso unavyoweza kuonyesha dalili za figo kuanza kuathirika | 0 | 10 | 25-08-2026 |