Soma zaidi...
Prime
Alhamisi, Agosti 27, 2026

Dar es Salaam. Baada ya kufukuzwa uanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ni njia mbili pekee ndizo zilizobaki kwa Dk Emmanuel Nchimbi, kurejea ndani ya chama hicho.
Taarifa ya Dk Nchimbi kufukuzwa uanachama, ilitangazwa usiku wa Agosti 26, 2026 na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Asha-Rose Migiro, baada ya vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu (NEC) Taifa, vilivyoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
"Kwa kauli moja Kamati Kuu ya CCM, imepitisha ndugu Nchimbi afukuzwe uanachama kwa mujibu wa kanuni zetu. Kwa hiyo tunapenda kuwafahamisha wanachama wote wa CCM na wananchi kwa ujumla kwamba CCM imefikia uamuzi huo.
“Kuanzia hivi sasa ndugu Nchimbi amefukuzwa uanachama na sio mwanachama tena wa Chama cha Mapinduzi, pokeeni taarifa hiyo," alisema Dk Migiro.
Alisema vikao hivyo vilijadili suala la nidhamu na maadili lililokuwa linamkabili Dk Nchimbi, baada ya kuzingatia taarifa zote zilizokuwepo imethibitika kuwa Katiba ya CCM imekiukwa.
Anarudije?
Njia anazoweza kuzitumia Dk Nchimbi kurudi chamani ya kwanza ni kukata rufaa kupinga kufutwa kwake uanachama. Hapa atatumia Kifungu cha 8 cha Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM, kinachompa haki ya kukata rufaa kama hakuridhishwa na adhabu iliyotolewa kwa makosa ya ukiukwaji maadili.
“Mwanachama au kiongozi yeyote ambaye hataridhishwa na adhabu iliyotolewa kwa makosa ya ukiukwaji wa maadili atakuwa na haki ya kukata rufaa kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa,” inaeleza kanuni hiyo.
Njia ya pili kwa Dk Nchimbi, kurejea ndani ya CCM inafafanuliwa katika Ibara ya 13(3) ya Katiba ya CCM. Kwa mujibu wa ibara hiyo, mwanachama aliyefukuzwa uanachama anapotaka kujiunga na CCM tena, itabidi aombe upya na atapeleka ombi lake ama katika Halmashauri Kuu ya wilaya au kikao kilichomfukuza.
“Mwanachama aliyeachishwa au kufukuzwa uanachama akitaka kujiunga tena katika CCM, itabidi aombe upya, na atapeleka maombi yake hayo ama katika Halmashauri Kuu ya Wilaya ama kikao kilichomwachisha au kumfukuza uanachama,” inaeleza kanuni ya chama hicho.
Njia hiyo, aliwahi kupita aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CCM Tanzania (UWT), Sophia Simba, alipofukuzwa uanachama Machi 2017 kwa makosa ya usaliti katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Baada ya kufukuzwa, Novemba mwaka huohuo aliofukuzwa 2017, alimwandikia barua Mwenyekiti wa CCM Taifa wa wakati huo, hayati John Magufuli ya kuomba msamaha.
Hayati Mgufuli, aliwasilisha ombi la Sophia mbele ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), nayo ikaridhia kumsamehe na kumrejeshea uanachama wake.
Adhabu ya Nchimbi kikanuni
Kifungu cha 8 cha Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM, kinaweka wazi adhabu za chama hicho kwa makada wake, huku kufukuzwa uanachama ikiwa ni adhabu kubwa zaidi.
Kwa mujibu wa kanuni hiyo, adhabu ya kufukuzwa uanachama aliyopewa Dk Nchimbi, inatolewa kwa mwanachama anayegundulika na makosa makubwa ya itikadi yanayoathiri uhai wa chama na ambaye ameshindwa huko nyuma kujirekebisha hata baada ya adhabu ya karipio.
“Basi Kamati Kuu itapendekeza mwanachama huyo afukuzwe uanachama na itapeleka shauri hili mbele ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa uamauzi wa mwisho,” inaeleza kanuni hiyo.
Kanuni hiyo, inaeleza kosa kubwa kuliko yote katika CCM ni kukisaliti chama na kukiweka katika hali ama ya kushindwa katika uchaguzi wa dola au kunuka mbele ya umma, anayeshirikiana na wapinzani kuchimba na kukivuruga.
“Huyo hawezi kukubalika kuwa miongoni mwetu. Afukuzwe katika chama. Kwa hiyo, ikithibitika kuwa mwanachama huyo anayatenda hayo kwa makusudi basi atakuwa amefukuzwa daima,” inaeleza kanuni hiyo.
Namna nyingine ya kufukuzwa uanachama, kanuni inasema ikithibitika kuwa mwanachama ametenda hayo ama kwa ujinga au kwa bahati mbaya basi adhabu yake ya kuangaliwa itakuwa miezi 48 na zote hizo zitatangazwa hadharani.
Mbali na kufukuzwa uanachama, Dk Nchimbi Agosti 25, 2026 alimwandikia Rais Samia barua ya kujiuzulu umakamu wa Rais na mkuu huyo wa nchi akaridhia.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Kinachofuata kwa Dk Nchimbi | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 2 | Bunge kumthibitisha Ndejembi leo | 0 | 10 | 28-08-2026 |
| 3 | Utata ukomo umakamu wa rais wa Nchimbi, wanasheria watofautiana | 0 | 8.4 | 27-08-2026 |
| 4 | Ndejembi awakuna wadau, apewa angalizo | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 5 | Jaji Warioba afichua alichozungumza na Dk Nchimbi kabla, baada ya kujiuzulu | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 6 | UWT: Hakuna mwanachama aliye juu ya CCM | 0 | 10 | 28-08-2026 |
| 7 | Uso unavyoweza kuonyesha dalili za figo kuanza kuathirika | 0 | 10 | 25-08-2026 |
| 8 | Mpinzani wa Hichilema ashikiliwa kwa tuhuma za uhaini | 0 | 8.9 | 28-08-2026 |
| 9 | Chadema cracks down on leaders who accused Heche | -2 | 6 | 11-07-2026 |
| 10 | Zambia's Hichilema leads presidential vote count | 0 | 10.99 | 16-08-2026 |