Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Serikali yataja sababu ya kuja na chanjo ya polio

Дата публикации: 28-08-2026 14:44:19

Soma zaidi...

Основное содержимое страницы с новостью.

By  Herieth Makwetta

Mwandishi wa habari

Mwananchi

Muktasari:
  • Yawasisitiza wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao walio chini ya umri wa miaka 10 wanapata chanjo hiyo, kwa kuwa uwepo wa virusi katika mazingira ni tishio linalohitaji hatua za haraka za kinga.

Dar es Salaam. Serikali imesema kampeni ya chanjo ya polio inayolenga watoto zaidi ya milioni 6.5 nchini imeanzishwa baada ya kubainika kwa virusi vya ugonjwa huo katika sampuli za majitaka mkoani Mwanza.

Hatua hiyo inalenga kuzuia virusi hivyo kuenea katika jamii na kusababisha mlipuko wa ugonjwa wa polio.

Kampeni hiyo inatekelezwa katika mikoa minane ambayo ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kilimanjaro, Manyara, Mara, Pwani na Tanga. Ilianza jana Alhamisi, Agosti 27, 2026, na inatarajiwa kukamilika Agosti 30, 2026.

Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa, Agosti 28, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Dk Georgina Joachim, amesema kampeni hiyo inalenga kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya polio nchini.

“Lengo la kampeni hii ni kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya polio baada ya kubainika kwa virusi hivyo katika sampuli za majitaka katika mazingira mkoani Mwanza,” amesema.

Hata hivyo, Dk Joachim amesema hadi sasa hakuna mtoto aliyethibitika kuwa na ugonjwa wa polio nchini, akisisitiza kuwa kubainika kwa virusi hivyo katika mazingira ni tishio linalohitaji hatua za haraka za kinga.

Amesema kampeni hiyo ni mwendelezo wa hatua zilizochukuliwa na Serikali katika awamu ya kwanza ya utoaji chanjo katika baadhi ya mikoa, ikiwemo Mwanza, kwa lengo la kuzuia maambukizi kabla hayajasababisha ugonjwa kwa watoto.

Dozi mbili

Chanjo hiyo ya matone itatolewa kwa dozi mbili, ambapo dozi ya kwanza inatolewa kuanzia Agosti 27 hadi 30, huku dozi ya pili ikitarajiwa kutolewa kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba 2, 2026.

Dk Joachim amesema utoaji wa dozi zote mbili ni muhimu ili watoto walengwa wapate kinga inayohitajika dhidi ya ugonjwa huo.

Amesema katika kuhakikisha watoto wote wanafikiwa, chanjo hiyo inatolewa kwa njia ya nyumba kwa nyumba, shuleni, vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo yenye mikusanyiko ya watu.

Maeneo mengine yanayolengwa ni nyumba za ibada, magulio, minada na vituo vya mabasi.

Kampeni hiyo inafanyika kwa wakati mmoja katika mikoa yote iliyotajwa, huku utoaji wa chanjo ukiwa umeanza jana.

Mmoja wa wazazi waliopeleka watoto wake katika Kituo cha Afya Tabata Segerea, Jenifer Peter, amesema ameona umuhimu wa kuwapatia chanjo watoto wake watatu kutokana na kufahamu madhara ya ugonjwa huo.

“Polio humfanya mtoto kuwa mlemavu au anaweza kufariki kabisa. Ni muhimu kuwakinga na daktari ameniambia hakuna madhara ya kurudia chanjo,” amesema.

Tishio kutoka nje

Tishio la polio pia linahusishwa na uwepo wa ugonjwa huo katika baadhi ya nchi jirani.

Malawi ni miongoni mwa nchi zilizowahi kuripoti ugonjwa huo, ikiwemo kisa kilichotangazwa mwaka 2022 baada ya kubainika kwa Wild Poliovirus. Hali hiyo ilisababisha nchi za ukanda huo, ikiwemo Tanzania, kuimarisha ufuatiliaji na kampeni za chanjo.

Tanzania imeendelea kuchukua hatua za kuzuia kurejea kwa polio baada ya kuripoti kisa cha mwisho cha ugonjwa huo mwaka 1996 katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.

Hatua hizo zimeendelea kuwa muhimu kutokana na uwepo wa virusi vya polio katika baadhi ya nchi za Afrika pamoja na mwingiliano wa kijamii unaovuka mipaka.

Hata hivyo, kampeni hii inafanyika wakati Tanzania ikiendelea kuimarisha ufuatiliaji wa polio kupitia mfumo wa uchunguzi wa mazingira, unaosaidia kubaini uwepo wa virusi kabla ya wagonjwa kuonekana.

Hatua hiyo inaendana na mikakati ya kimataifa ya kukabiliana na tishio la polio, hususan katika maeneo yenye mwingiliano mkubwa wa watu na nchi nyingine.

Wizara ya Afya imesisitiza kuwa ushirikiano wa wazazi, walezi, viongozi wa jamii na wahudumu wa afya ni muhimu katika kuhakikisha watoto wote walio chini ya miaka 10 wanapata chanjo katika awamu zote mbili za kampeni.

Polio ni nini?

Polio ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vinavyoweza kuingia mwilini baada ya mtu kutumia chakula au maji yaliyochafuliwa na kinyesi chenye virusi hivyo.

Virusi hivyo hushambulia mfumo wa fahamu na vinaweza kusababisha kupooza kwa ghafla kwa kiungo kimoja au zaidi cha mwili. Ulemavu huo unaweza kuwa wa kudumu na wakati mwingine kusababisha kifo.

Dalili za awali zinaweza kuwa homa, uchovu, maumivu ya kichwa, kutapika, kukakamaa kwa shingo na maumivu ya viungo.

Dk Joachim amesema kwa kuwa polio haina tiba, chanjo ndiyo njia kuu ya kuzuia ugonjwa huo.

Amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo wakati timu za afya zinapowafikia.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Dk Nchimbi alivyopigwa chenga ya mwili01028-08-2026
2Kilio cha abiria Stendi ya Magufuli chaanza kutatuliwa01028-08-2026
3Lissu alivyohitimisha utetezi wake katikati ya mapingamizi ya Jamhuri08.2628-08-2026
4Mnyika ajitwisha dhamana mkutano Lissu aliodaiwa kufanya uhaini01028-08-2026
5Warioba aeleza wasiwasi wake kupatikana Katiba mpya 202902028-08-2026
6CAG Kichere azishukia halmashauri tano Mara, atishia...06.0928-08-2026
7DRC authorities begin vaccination campaign against Ebola010.4128-08-2026
8В ДРК медиков начали прививать от Эболы вакциной от другого штамма09.128-08-2026
9В ДР Конго начали вакцинацию против лихорадки Эбола013.0628-08-2026
10Reuters: США не поставят Евросоюзу вакцины AstraZeneca в ближайшее время0011-03-2021

Классификация: Общество. Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 8.26. Источник: www.mwananchi.co.tz.