Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Lissu alivyohitimisha utetezi wake katikati ya mapingamizi ya Jamhuri

Дата публикации: 28-08-2026 12:15:55

Soma zaidi...

Основное содержимое страницы с новостью.

Muktasari:
  • Lissu amefunga ushahidi wake leo Ijumaa, Agosti 28, 2026 kwa kutoa ufafanuzi wa majibu ya baadhi ya maswali ya dodoso aliyoulizwa na waendesha mashtaka wakati wa hatua ya pili ya ushahidi wake.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amehitimisha ushahidi wake wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, baada ya kutumia siku tano kutoa ushahidi.

Lissu amefunga ushahidi wake leo Ijumaa, Agosti 28, 2026, kwa kutoa ufafanuzi wa majibu ya baadhi ya maswali ya dodoso aliyoulizwa na waendesha mashtaka. wakati wa hatua ya pili ya ushahidi wake.

Hata hivyo, wakati akitoa ufafanuzi huo, Lissu amekumbana na mapingamizi ya mara kwa mara kutoka kwa upande wa mashtaka kuhusu utaratibu wa kutoa ufafanuzi wa majibu ya maswali aliyokuwa ameulizwa.

Mapingamizi hayo yameibua mvutano wa hapa na pale kati ya Lissu na waendesha mashtaka, wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga.

Mara kadhaa Katuga amepinga ufafanuzi uliokuwa ukitolewa na Lissu, akidai haukuwa wa lazima kwa sababu swali alilokuwa ameulizwa lilikuwa limejibiwa kikamilifu katika ushahidi wake wa awali.

Katika baadhi ya mapingamizi, Wakili Katuga pia alidai Lissu alikuwa akitoa maelezo mapya ambayo hayakuhusiana moja kwa moja na swali aliloulizwa.

Amesema endapo mshtakiwa akiendelea kutoa ushahidi mpya, Jamhuri ingelazimika kuomba fursa ya kumhoji tena kuhusu maelezo hayo, jambo ambalo lingeongeza muda wa kesi.

Baadhi ya mapingamizi hayo yamekubaliwa na mahakama, huku Lissu akitakiwa kuzingatia mipaka ya hatua hiyo ya ufafanuzi.

Katika baadhi ya maswali, Lissu amekubaliana na mapingamizi ya upande wa mashtaka na kubadilisha ufafanuzi aliokuwa ameanza kuutoa au kuachana nao.

Ushahidi wa siku tano

Lissu ambaye pia ni mwanasheria na Wakili, alianza kutoa ushahidi wake wa utetezi Agosti 21, 2026, baada ya mahakama kumkuta ana kesi ya kujibu.

Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu akiwasili katika Mahakama Kuu Masijala ndogo ya Dar es Salaam leo Agost 28, kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili mwenyekiti huyo ambapo leo kesi hiyo inaendelea kwa maswali ya dodoso. Picha na Said Powa

Uamuzi huo ulitolewa baada ya Mahakama Kuu kuzingatia ushahidi wa mashahidi 17 wa upande wa Jamhuri.

Katika ushahidi wake wa msingi, Lissu alitumia siku tatu akijibu tuhuma zinazomkabili na kuchambua ushahidi uliotolewa na mashahidi wa mashtaka.

Pamoja na mambo mengine, alieleza mtazamo wake kuhusu aina ya mashahidi wa Jamhuri na ushahidi walioutoa, akidai upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha shtaka linalomkabili.

Alidai pia kuwa upelelezi wa kesi hiyo haukufanyika kwa kiwango kinachostahili.

Baada ya kumaliza ushahidi wake wa msingi Jumatano, Agosti 26, Lissu aliingia katika hatua ya pili ya ushahidi, ambayo ilikuwa ni kujibu maswali ya dodoso kutoka kwa waendesha mashtaka.

Katika hatua hiyo, Jamhuri ilimuuliza maswali mbalimbali kuhusu mambo aliyoyaeleza katika ushahidi wake wa msingi.

Mahojiano hayo yamekamilika leo Ijumaa, Agosti 28, na Lissu amepewa fursa ya mwisho ya kufafanua baadhi ya majibu aliyoyatoa.

Kwa kiasi kikubwa, katika hatua hiyo Lissu amesisitiza majibu aliyokuwa ameyatoa awali au kuongeza maelezo mafupi pale alipohitaji kufanya hivyo.

Baada ya kukamilisha hatua hiyo, Lissu amefunga rasmi ushahidi wake binafsi kama mshtakiwa na shahidi wa kwanza wa utetezi.

Mashahidi wengine waanza

Baada ya Lissu kumaliza kutoa ushahidi, mashahidi wengine wa utetezi ambao hawajawekewa pingamizi, wameanza kupewa nafasi ya kutoa ushahidi wao wa kumtetea.

Miongoni mwa mashahidi hao ni viongozi wa Chadema ambao wameorodheshwa na upande wa utetezi, wa kwanza akiwa Katibu Mkuu John Mnyika.

Hata hivyo, mbali na mashahidi wa Chadema, katika orodha ya mashahidi 11 waliotajwa na Lissu, wapo viongozi wakuu wa Serikali na wastaafu ambao Jamhuri imepinga kuitwa mahakamani.

Miongoni mwao ni Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais mstaafu Dk Philip Mpango, Waziri Mkuu mstaafu Kassim Majaliwa pamoja na baadhi ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Waendesha mashtaka wamepinga mashahidi hao kuitwa, miongoni mwa hoja zao ikiwa ni kwamba sheria haiwalazimishi baadhi ya viongozi, hususan Rais, kufika mahakamani kutoa ushahidi.

Lissu amepinga hoja hizo, akisema Sheria ya Masuala ya Rais inampa Rais kinga ya kutolazimika kufika mahakamani kutoa ushahidi, lakini pia inaweka utaratibu wa kumfikishia wito na uamuzi unabaki wa kwake.

Amesema viongozi wengine wastaafu na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama hawana kinga hiyo, hivyo wanapaswa kuitwa na kutoa ushahidi.

Baada ya kusikiliza hoja hizo, mahakama ilisema itatoa uamuzi wake baadaye.

Lissu anakabiliwa na shtaka la uhaini kinyume na Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code), Rekebu ya mwaka 2023.

Anadaiwa kuwa Aprili 3, 2025, akiwa raia wa Tanzania, kwa nia ya uchochezi alishawishi umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Mnyika ajitwisha dhamana mkutano Lissu aliodaiwa kufanya uhaini01028-08-2026
2Serikali yataja sababu ya kuja na chanjo ya polio08.2628-08-2026
3Ijue siri ya kisukari iliyojificha kwenye wali, ugali01007-08-2026
4Kilio cha abiria Stendi ya Magufuli chaanza kutatuliwa01028-08-2026
5Dk Nchimbi alivyopigwa chenga ya mwili01028-08-2026
6Migogoro inapogeuka rafiki wa ndoa01009-08-2026
7Aliyedaiwa kuchoma moto mahakama Moshi akamatwa kwenye Maulidi01026-08-2026
8Warioba aeleza wasiwasi wake kupatikana Katiba mpya 202902028-08-2026
9Rais Samia ataka Tanzania, Misri kuongeza biashara05.5228-08-2026
10Mashindano ya Feassa yafunga shule Morogoro Mjini, ikiibua sintofahamu01010-08-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 8.26. Источник: www.mwananchi.co.tz.