Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Utata ukomo umakamu wa rais wa Nchimbi, wanasheria watofautiana

Дата публикации: 27-08-2026 16:09:31

Soma zaidi hapa...

Основное содержимое страницы с новостью.

Prime

Alhamisi, Agosti 27, 2026

By  Mwandishi Wetu

Mwananchi Digital

Mwananchi

Muktasari:
  • Kuondolewa kwa Dk Emmanuel Nchimbi katika nafasi ya makamu wa rais kumeisha mara moja baada ya kupoteza uanachama wa CCM au unaendelea hadi Septemba 4? Wanasheria wanajadili hili.

Dar es Salaam. Wanasheria wamegawanyika kuhusu muda ambao Dk Emmanuel Nchimbi kisheria ataacha kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania baada ya kufukuzwa kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), siku chache kabla ya kutekelezwa aliyoyaandika katika taarifa yake ya kujiuzulu.

Dk Nchimbi aliwasilisha taarifa ya kujiuzulu ambayo inaeleza kwamba atajiuzulu rasmi kuanzia Septemba 4, 2026, ombi ambalo baadaye lilikubaliwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Hata hivyo, CCM ilimfukuza Dk Nchimbi katika chama hicho Agosti 26 na kumteua Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi kuwa Makamu wa Rais mteule, hali iliyoibua maswali iwapo muda wa Dk Nchimbi katika nafasi hiyo umeisha mara moja baada ya kupoteza uanachama wa CCM au unaendelea hadi Septemba 4.

Akizungumzia suala hilo, Wakili Paul Kisabo kutoka Muungano wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), amesema Dk Nchimbi bado ni Makamu wa Rais hadi Septemba 4.

Amesema Katiba inaweka uanachama wa chama cha siasa kuwa moja ya sifa za mtu kuwa Makamu wa Rais, lakini haijaeleza moja kwa moja kuwa kupoteza uanachama wa chama kunamaliza moja kwa moja nafasi ya Makamu wa Rais.

Akiwa na mtazamo tofauti na Kisabo, Wakili Peter Majanjara amesema Dk Nchimbi aliacha kuwa na sifa za kushikilia nafasi hiyo mara moja baada ya kufukuzwa CCM.

“Endapo amekoma kuwa mwanachama wa chama cha siasa kwa kufukuzwa, basi hana tena sifa za kikatiba kuwa Makamu wa Rais, hivyo muda wake wa kushikilia nafasi hiyo unaishia hapo,” amesema.

Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi amesema kumvua Dk Nchimbi uanachama hakumaanishi kwamba ameacha kuwa Makamu wa Rais, kwa sababu Katiba haijaweka kufukuzwa uanachama kama sababu ya moja kwa moja ya kuacha kuwa makamu wa rais.

“Kwa kuwa Balozi Nchimbi aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwake kwa Rais na kwamba kutaanza Septemba 4, 2026, na Rais akakubali kujiuzulu huko kuanzia tarehe hiyo, hivyo anaendelea kuwa Makamu wa Rais hadi Septemba 4, 2026 isipokuwa kama kuna utaratibu mwingine utakaofuatwa na Bunge kikatiba na si vinginevyo,” amesema.

Mwabukusi amesema CCM inaweza kumvua uanachama, lakini haiwezi kumvua madaraka ya Makamu wa Rais, isipokuwa kwa msingi na sababu zilizoainishwa katika Katiba.

“Hapa ndipo penye utata wa kikatiba unaohitaji tafsiri ya maudhui ya Ibara ya 47 na 50. Ni jambo ambalo linahitaji tafsiri muhimu ya kisheria na hili linaweza kufanyika mahakamani pekee,” amesema.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Ndejembi awakuna wadau, apewa angalizo01027-08-2026
2Kinachofuata kwa Dk Nchimbi01027-08-2026
3Hivi ndivyo Dk Nchimbi anavyoweza kurudi CCM01027-08-2026
4Tamu, chungu kupigana busu kiafya0002-07-2026
5Bunge kumthibitisha Ndejembi leo01028-08-2026
6Jaji Warioba afichua alichozungumza na Dk Nchimbi kabla, baada ya kujiuzulu01027-08-2026
7UWT: Hakuna mwanachama aliye juu ya CCM01028-08-2026
8Hii hapa mianya maandalizi ya walimu tarajali0030-06-2026
9Yanayowasubiri wahitimu mitaani0020-07-2026
10Wahadhiri vyuo vikuu watoa tamko kupinga kamatakamata0520-07-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 8.4. Источник: www.mwananchi.co.tz.