Soma hapa...
Dodoma. Bunge la Tanzania leo Ijumaa, Agosti 28, 2026 litapokea na kumthibitisha uteuzi wa Deogratius Ndejembi kuwa Makamu wa Rais.
Kwa mujibu wa orodha za shughuli za Bunge leo, pamoja na mambo mengine, wabunge watapata fursa hiyo kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.
Jumatano ya Agosti 27, 2026, Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ilimpendekeza Ndejembi ambaye ni Waziri wa Nishati kuwa Makamu wa Rais.
Ndejembi ambaye pia ni Mbunge wa Chamwino, Mkoa wa Dodoma anakwenda kuchukua nafasi ya Dk Emmanuel Nchimbi ambaye ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo.
Baada ya Bunge kudhibitisha, itabaki kuapishwa na kuanza majukumu mapya ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa taarifa ya Bunge, Ndejembi alianza elimu ya msingi Cannon Andrea kuanzia mwaka 1988–1995, kisha akasoma sekondari ya Kigurunyembe mwaka 1996–1998 na Merton College 2002–2004.
Kati ya mwaka 2006–2009 alisoma Shahada ya International Relations katika University of Lincoln nchini Uingereza. Baadaye, mwaka 2009–2012, alisoma Advanced Diploma katika Institute of Administrative Management.
Kabla ya kuwa mbunge, Ndejembi aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Dodoma. Mwaka 2020, alipitishwa na CCM kuwa mgombea wa ubunge wa Jimbo la Chamwino.
Amewahi kuhudumu unaibu Waziri Ofisi ya Rais, (Utumishi wa Umma na Utawala Bora) kabla ya kuingia kwenye nafasi ya uwaziri kamili.
Julai 2024, Rais Samia alimteua Ndejembi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya kushika Umakamu wa Rais Ndejembi alikuwa Waziri wa Nishati.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Ndejembi awakuna wadau, apewa angalizo | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 2 | Hivi ndivyo Dk Nchimbi anavyoweza kurudi CCM | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 3 | Kinachofuata kwa Dk Nchimbi | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 4 | UWT: Hakuna mwanachama aliye juu ya CCM | 0 | 10 | 28-08-2026 |
| 5 | Jaji Warioba afichua alichozungumza na Dk Nchimbi kabla, baada ya kujiuzulu | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 6 | Utata ukomo umakamu wa rais wa Nchimbi, wanasheria watofautiana | 0 | 8.4 | 27-08-2026 |
| 7 | Migogoro inapogeuka rafiki wa ndoa | 0 | 10 | 09-08-2026 |
| 8 | Ijue siri ya kisukari iliyojificha kwenye wali, ugali | 0 | 10 | 07-08-2026 |
| 9 | Zacharia: Mhitimu la saba anayetamba kwenye uhandisi | 0 | 10 | 25-08-2026 |
| 10 | UCHAMBUZI WA MJEMA: Tusijidanganye, tunahitaji maandalizi haya kabla ya 2030 | 0 | 18.33 | 27-08-2026 |