Вход на сайт

Просмотр новости

Найдите то, что Вас интересует

Tiba asili si uchawi, wananchi waelimishwa

Дата публикации: 27-08-2026 17:30:12

Wananchi wametakiwa kuondokana na dhana potofu ya kuitazama tiba asili kama uchawi, badala yake waitambue kuwa ni sehemu ya maarifa ya afya yanayotumika kuchunguza, kutibu na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali za kiafya.

Основное содержимое страницы с новостью.

Alhamisi, Agosti 27, 2026

Mkurugenzi Msaidizi wa tiba asili na tiba mbadala, Dk Winifrida Kidima akizungumza kuhusu maadhimisho ya wiki ya tiba asili ya mwafrika yanayofanyika jijini Mbeya.

By  Sadam Sadick

Mwananchi Communications Limited

Muktasari:
  • Maadhimisho ya wiki ya tiba asili yameanza Agosti 25 mikoa yote nchini, ambapo kilele chake itakuwa Agosti 31 yakifanyika kitaifa mkoani Mbeya.

Mbeya. Wananchi wametakiwa kuondokana na dhana potofu ya kuitazama tiba asili kama uchawi, badala yake waitambue kuwa ni sehemu ya maarifa ya afya yanayotumika kuchunguza, kutibu na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali za kiafya.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi, Agosti 27, 2026 jijini Mbeya katika maadhimisho ya Wiki ya Tiba Asili ya Mwafrika, huku ikielezwa kuwa takribani asilimia 60 ya Watanzania hutumia huduma za tiba asili zinazotokana na mimea, madini na baadhi ya mabaki ya wanyama.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoka Wizara ya Afya, Dk Winifrida Kidima amesema moja ya malengo ya maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu nafasi na mchango wa tiba asili katika huduma za afya.

Amesema bado kuna wananchi wenye mtazamo kuwa tiba asili ni sawa na uchawi, hali inayosababisha baadhi yao kushindwa kutambua kuwa huduma hizo zinatokana na maarifa ya ndani yaliyorithishwa kutoka kizazi hadi kizazi, pamoja na maarifa mengine yanayofundishwa katika taasisi za elimu.

“Bado kuna mtazamo kuwa tiba asili ni uchawi badala ya kujua kuwa ni maarifa ya ndani yanayotumika kutibu, kuchunguza na kutatua changamoto za afya. Tunatumia miti dawa, madini na mabaki ya wanyama kutengeneza dawa,” amesema Dk Kidima.

Amesema takribani asilimia 60 ya Watanzania hutumia huduma za tiba asili, akisisitiza kuwa huduma hizo ni sehemu ya huduma za afya zinazotokana na maarifa ya jamii na yale yanayopatikana kupitia mafunzo rasmi.

Kwa mujibu wa Dk Kidima, sekta ya tiba asili inahusisha makundi mbalimbali, yakiwamo watengenezaji wa dawa, watoa huduma, wadau wa tiba asili, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na watoa huduma jumuishi katika hospitali 14 za rufaa nchini.

Amesema Wizara ya Afya inaendelea kufanya tafiti na kujifunza ili kuhakikisha maendeleo ya tiba asili yanaendana na taratibu za nchi, sambamba na kufuata miongozo na mkakati wa Shirika la Afya Duniani (WHO) katika utekelezaji wa afua za tiba asili.

“Wizara tunayo kazi ya kutoa huduma na kujenga uelewa kwa jamii. Ujumuishaji unaendelea hatua kwa hatua na kwa sasa ni mwaka wa pili tukifuatilia miongozo ya WHO katika utekelezaji wa afua za afya,” amesema.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk Elizabeth Nyema amesema Serikali itaendelea kuitambua tiba asili kama sehemu muhimu ya rasilimali za afya, maarifa ya jamii na urithi wa utamaduni wa Watanzania.

Amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha mchango wa tiba asili katika huduma za afya unaendelezwa kwa kuzingatia utafiti wa kisayansi, udhibiti, uhakiki wa ubora na ujumuishaji unaofaa katika mfumo wa afya.

“Usalama wa wananchi na ushahidi wa kisayansi vitaendelea kuwa msingi wa maendeleo ya tasnia hii hapa nchini. Serikali itaendelea kusimamia hilo kwa manufaa ya nchi,” amesema Dk Nyema.

Kwa upande wake, Sebastian Kazi amesema kutokujumuishwa kikamilifu kwa tiba asili katika mfumo rasmi wa huduma za afya ni miongoni mwa sababu zinazochangia baadhi ya wananchi kuendelea kuiona kama eneo la uchawi.

Amesema baadhi ya watoa huduma za tiba asili hawajawa wazi katika utoaji wa huduma zao, jambo linalochangia kuwepo kwa dhana potofu.

“Mtu anaweza kuamini kuwa kwenda kwa mganga wa jadi ni pale tu anaposhindwa kutibiwa kwa tiba za kisasa. Pia, baadhi ya watoa huduma wamekuwa wakifanya kazi kwa kujificha, ndiyo maana kuna mtazamo huo tofauti na uhalisia wa tiba asili,” amesema Kazi.

Maadhimisho hayo yameweka mkazo katika umuhimu wa kuendeleza tiba asili kwa kuzingatia usalama wa wananchi, utafiti wa kisayansi na ubora wa huduma, huku jamii ikihamasishwa kuondokana na mitazamo inayochanganya maarifa ya tiba asili na imani za uchawi.

Схожие новости

#Наименование новостиТональностьИнформативностьДата публикации
1Ukweli kuhusu maziwa kwenye matibabu 06.6628-08-2026
2Afya bora uzeeni inaanzia kwenye ujana06.8228-08-2026
3Ambulance kupunguza changamoto za rufaa Kibaha Vijijini05.2625-08-2026
4Matumaini mapya kwa waliojifungua kwa upasuaji08.5225-08-2026
5Elimu ya magonjwa yasiyoambukiza ianzie shuleni06.0128-08-2026
6Malipo ya kidijitali yanavyobadili utamaduni wa kifedha Zanzibar06.3427-08-2026
7Ndejembi awakuna wadau, apewa angalizo01027-08-2026
8Utata ukomo umakamu wa rais wa Nchimbi, wanasheria watofautiana08.427-08-2026
9Utafiti wafichua uhusiano wa ulaji, VVU na hatari ya kisukari05.0628-08-2026
10Kinachofuata kwa Dk Nchimbi01027-08-2026

Классификация: . Схожих патентов: 0. Схожих новостей: 10. Тональность: 0. Информативность: 6.66. Источник: www.mwananchi.co.tz.