Soma hapa...
Jumatano, Agosti 26, 2026

Dar es Salaam. Bei ya dhahabu katika soko la dunia imepanda kwa kasi mwezi huu, baada ya kushuka kwa zaidi ya asilimia 11 mwezi Juni, hali inayowapa matumaini wachimbaji wadogo wanaonufaika na mabadiliko ya bei ya madini hayo katika soko la kimataifa.
Kwa mujibu wa kampuni ya habari na uchambuzi wa masoko ya dhahabu, Kitco, na London Bullion Market Association (LBMA), bei ya dhahabu ilikuwa Dola 4,532.03 za Marekani (Sh11.998 milioni) kwa wakia mwishoni mwa Mei, kabla ya kushuka hadi dola 4,022.29 za Marekani (Sh10.649 milioni) mwishoni mwa Juni, sawa na punguzo la takribani asilimia 11.2.
Hata hivyo, bei hiyo ilianza kuimarika Julai na kufikia Dola 4,049.83 (Sh10.721 milioni) kwa wakia mwishoni mwa mwezi huo, ongezeko lililoshuhudiwa zaidi Agosti, ambapo bei ya dhahabu katika soko ilifikia Dola 4,624.87 (Sh12.244 milioni) kwa wakia Jumanne, Agosti 25, kwa mujibu wa Kitco.
Bei hiyo ya Agosti 25 ni ongezeko la takribani asilimia 14.2 ikilinganishwa na mwisho wa Julai na imepita kwa takribani asilimia mbili bei iliyokuwepo mwishoni mwa Mei. Hii ina maana kuwa dhahabu imerejesha zaidi ya hasara iliyopata mwezi Juni.
Kupanda kwa bei hiyo kumechangiwa na mambo mbalimbali, ikiwamo kudhoofika kwa dola ya Marekani, mabadiliko ya matarajio kuhusu viwango vya riba nchini humo na kuongezeka kwa mahitaji ya dhahabu kama mali salama wakati wa vipindi vya sintofahamu za kiuchumi na kisiasa.
Kwa kawaida, dola inapodhoofika dhidi ya sarafu nyingine, dhahabu huwa na mvuto zaidi kwa wanunuzi wanaotumia sarafu hizo kwa sababu gharama ya kununua dhahabu hupungua, na kinyume chake, viwango vya juu vya riba vinaweza kupunguza mvuto wa dhahabu kwa kuwa madini hayo hayatoi riba kama ilivyo kwa baadhi ya uwekezaji wa kifedha.
Akizungumzia suala hilo, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba, amesema mwenendo wa bei ya dhahabu umeathiriwa pia na hali ya kisiasa duniani, ikiwamo migogoro ya Mashariki ya Kati na mabadiliko ya bei ya mafuta.
“Soko la dhahabu ni miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa na mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati na kupanda kwa bei za mafuta,” amesema.
Amesema matarajio kuhusu mabadiliko ya viwango vya riba nchini Marekani yamekuwa yakichochea baadhi ya wawekezaji kuongeza umiliki wa dhahabu kutokana na uwezo wake wa kutumika kama kinga dhidi ya hatari wakati wa kutokuwa na uhakika katika uchumi na siasa.
Tutuba pia amesema kuna uhusiano kati ya thamani ya dola ya Marekani na bei ya dhahabu, akieleza kuwa dola inapokuwa imara, bei ya dhahabu huwa na mwelekeo wa kushuka, huku dola inapodhoofika, bei ya dhahabu ikielekea kupanda.
Kwa upande mwingine, ununuzi unaoendelea kufanywa na benki kuu duniani umeongeza mahitaji ya dhahabu, huku baadhi ya taasisi hizo zikitumia dhahabu kama sehemu ya kutofautisha na kusawazisha akiba zao.
Mchambuzi wa masuala ya fedha, Oscar Mkude, amesema mabadiliko ya bei ya dhahabu ni jambo la kawaida katika masoko ya bidhaa kutokana na mabadiliko ya mahitaji, uzalishaji na hali ya uchumi duniani.
“Mabadiliko ya bei, iwe inapanda au kushuka, ni jambo la kawaida katika soko. Kwa kiasi kikubwa huchochewa na mabadiliko ya bei na mahitaji, pamoja na matukio yanayoathiri mnyororo wa usambazaji,” amesema.
Amesema endapo bei itaendelea kupanda katika miezi ijayo, hali hiyo haitakuwa jambo la kushangaza, hasa iwapo changamoto katika uzalishaji na usambazaji zitaendelea sambamba na mahitaji makubwa.
Kwa wachimbaji wadogo, mabadiliko hayo ya bei yana maana ya moja kwa moja katika mapato yao, ambapo Nurath Athumani, mchimbaji mdogo kutoka Butundwe Luhuha katika mgodi wa Imalabuhabi, amesema wakati bei ya dhahabu inaposhuka, wachimbaji wanaweza kulazimika kusubiri kabla ya kuuza ili kupata bei nzuri.
“Bei ya dunia inaposhuka, tunalazimika kusubiri hadi ipande tena kabla ya kuuza. Tunapendelea kuuza wakati bei iko juu, lakini inaposhuka, tunahifadhi dhahabu hadi soko litakapokuwa zuri,” amesema.
| # | Наименование новости | Тональность | Информативность | Дата публикации |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Ndejembi awakuna wadau, apewa angalizo | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 2 | Ijue siri ya kisukari iliyojificha kwenye wali, ugali | 0 | 10 | 07-08-2026 |
| 3 | Bunge kumthibitisha Ndejembi leo | 0 | 10 | 28-08-2026 |
| 4 | Kinachofuata kwa Dk Nchimbi | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 5 | Mapato Stendi ya Magufuli yapaa | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 6 | Utata ukomo umakamu wa rais wa Nchimbi, wanasheria watofautiana | 0 | 8.4 | 27-08-2026 |
| 7 | Migogoro inapogeuka rafiki wa ndoa | 0 | 10 | 09-08-2026 |
| 8 | Jaji Warioba afichua alichozungumza na Dk Nchimbi kabla, baada ya kujiuzulu | 0 | 10 | 27-08-2026 |
| 9 | Hizi hapa sababu za kuwekeza kwa wasichana | 0 | 9.18 | 25-08-2026 |
| 10 | Lissu mahakamani kesi ya uhaini | 0 | 10 | 17-08-2026 |